Na, Egidia Vedasto,Misalaba Media,
Faida za mnyama kazi punda zimeendelea kuwa dhahiri na kupelekea kukubalika kitaifa na kimataifa imeelezwa.
Katika nchi ya Tanzania mnyama huyo hufugwa katika baadhi ya mikoa ikiwemo Dodoma, Singida Shinyanga, Geita, Arusha na Manyara. Katika mikoa hiyo jamii inayofuga wanyama hao inakiri kuwa utajiri upo iwapo punda atatunzwa na kuhudumiwa ipasavyo ili kutekeleza majukumu yake.
Kwa utafiti uliofanywa na mradi wa ustawi wa mnyama kazi punda ASPA kwa kushirikiana na Shirika la BROOKE EAST AFRIKA taarifa zinasema kuwa mnyama huyo kwa tawimu za mwaka 2018/2019 idadi ya punda ilikuwa 657,389 na ni wa pili kwa faida, si kwa kuuzwa bali faida hiyo ilionekana kwa kusaidia shughuli za uzalishaji kama kilimo, kubeba maji, kupeleka bidhaa sokoni, kubeba bidhaa migodini na nyinginezo.
Mradi wa ASPA umetoa mafunzo kwa Wanahabari Jijini Arusha namna mnyama huyo anasaidia kaya maskini kurahisisha kazi na kufika maeneo yasiyofikika kwa urahisi hususan maeneo yenye milima. Punda hutumika badala ya vyombo vya moto.
Akitoa mafunzo hayo Mkurugenzi mtendaji wa mradi huo Livingstone Masija amesema jamii baada ya kupata mafunzo namna ya kumtunza punda, idadi ya vifo imepungua, punda wameongezeka, magonjwa ya punda yamepungua.
Aidha amebainisha kuwa mazingira ya mnyama huyo yakiwa mazuri hufanya kazi kwa ufanisi, amesisitiza kuwa anatakiwa apewe chakula, mapumziko, atibiwe vidonda na kukaguliwa kila wakati.
"Kabla ya mradi huu kuanza jamii ilikuwa na fikra duni dhidi mnyama punda, kwani jamii haikumjali badala yake ilimtumikisha bila kujali haki zake za msingi. Tuliwafundisha wafugaji kuwa punda anatakiwa kuangaliwa mara kwa mara ili kubaini kama ana changamoto na kuwaepushia vifo visivyo vya lazima. amesema Masija.
Katika namna hiyohiyo Daktari Jastin Kirenga kutoka wizara ya mifugo na uvuvi amesema punda wanategemewa kwa usafiri licha ya kwamba kwenye orodha ya wanyama wafugwao majumbani amesahaurika.
Amesema katika baraza la washauri wa Waziri lililoundwa limeazimia kuhakikisha mnyama huyo anatambuliwa na kupatiwa haki zake ikiwemo chanjo, na dawa kama ilivyo kwa wanyama wengine.
Licha ya faida zake kuonekana waziwazi lakini serikali imekuwa haionyeshi kipaumbele kwa mnyama huyo licha ya taifa la China kuchangamkia bidhaa za punda kutengenezea dawa ya kikohozi, kuongeza damu, kuweka sawa mtiririko wa hedhi na kumfanya mtu asizeeke.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment