Na Belnardo Costantine, Misalaba MediaAfisa wa juu na msemaji wa kundi la waasi la M23, kanal Willy Ngoma ameuawa kwa shambulio la ndege nyuki "drone" ya jeshi la kongo karibu na Rubaya, katika Wilaya ya Masisi, Kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mashariki.Balozi na afisa mkuu wa M23 aliiambia Reuters kuwa msafara wa kanali Willy Ngoma ambaye ni Msemaji mkuu wa Kundi la waasi la AFC/M23 wa pamoja na maafisa wengine wa Kundi hilo umeshambiluwa saa 10 usiku jana jioni Kwa saa za jamhuri ya kidemokrasia ya congo (DRC)Aidha taarifa za Kifo chake kinakuja wakati wa mazungumzo ya kusitisha mapigano yanayoendelea nchini Qatar, ambapo serikali ya Kongo na M23 zimesaini makubaliano ya kuanzisha tume ya uangalizi inayojumuisha Marekani, Umoja wa Afrika, na Qatar.Hatahivyo inaelezwa Kwa kundi la M23, ambalo Umoja wa mataifa idai kuungwa mkono mkono na serikali ya Rwanda, linadhibiti sehemu kubwa za Kivu Kaskazini na Kusini, ikiwemo miji ya Goma na Bukavu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment