" WAZIRI MKUU APONGEZA JUHUDI KASI YA UJENZI MIRADI YA MAENDELEO JIJINI ARUSHA.

WAZIRI MKUU APONGEZA JUHUDI KASI YA UJENZI MIRADI YA MAENDELEO JIJINI ARUSHA.

Na, Egidia Vedasto,

Misalaba Media, Arusha.

Waziri mkuu nchini Dkt.Mwigulu Nchemba ameridhishwa na kasi iliyopo ya ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa Jijini Arusha.

Akiwa katika ziara yake unapotekelezwa mradi wa ujenzi wa stendi kuu ya mabasi eneo la Bondeni city iliyopo kata ya Olasiti ameelekeza ujenzi  wa barabara njia nne na kuelekeza kuanza matumizi ya  magari ya mwendokasi yanayotumia gesi na umeme ili kusapoti matumizi ya nishati safi.


"Miradi inayotekelezwa katika nchi italeta heshima kwa taifa letu na inadhihirisha ile kauli ya kazi na utu,  kwa sasa kila mmoja anaona mageuzi makubwa katika sekta ya afya hospitali za wilaya zimejengwa 119 na kufungwa vifaa vyote, vituo vya afya 649, zahanati zaidi ya 2700, vifaa vya kibingwa katika hospitali zote za mikoa na rufaa, si hivyo tu bali hata umeme imebaki historia nzuri kwamba umeme haukatiki tena na mengine mengi ikiwemo sekta ya elimu ambayo imekuwa na mageuzi makubwa".

Sambamba na hayo amewataka wakandarasi anbao wameshalipwa peza zao na serikali kuwalipa wafanyakazi wake bila kuwacheleweshea malipo yao.amesema vizimba wapewe watu wanaofanya biashara na sio kuwapa watu lengo la kukodishia wengine kwa gharama kubwa.

Vilevile amesikiliza kero za wananchi na kuzitatua, ameahidi kuendelea na zoezi hilo katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Waziri wa habari michezo sanaa na utamaduni Paul Makonda amempongeza Waziri mkuu kwa kuendelea kusikiliza kero za wananchi nchini na kuzipatia ufumbuzi.

Amemuomba asonge mbele na kasi hiyohiyo ili kujiwekea adhina mbinguni kwa kusaidia wananchi wanyonge.


Waziri Makonda amesema jijini arusha kuna miradi 52  imayotekelezwa na inazingatia ilani ya chama cha mapinduzi.

"Waziri mkuu ndio msimamizi wa TAMISEMI hivyo kila kinachotamkwa kitatendeka ikiwemo kukamilisha barabara za ndani zenye urefu wa kilometa 13 zinazojengwa 

 kwa kiwango cha lami ili kurahisisha mawasiliano kuelekea mashindano AFCON.

Katika namna hiyo hiyo mkuu wa mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla amepongeza juhudi za wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maendeleo katka mkoa wa arusha.

Ameahidi kushirikiana  na wadau mbalimbali kuhakikisha miradi hiyo  inakamilika kwa wakati kama ilivyoelekezwa.

Hata hivyo CPA Makalla ameonya juu ya migogoro isiyo ya lazima baina ya wafanya biashara na baadhi ya watumishi wasio waadilifu.

Post a Comment

Previous Post Next Post