
Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club imelazimishwa sare ya bila kufungana na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwa ushindani mkubwa na tahadhari za hali ya juu kutoka kwa pande zote mbili uliochezwa Februaria 25, 2026 jijini Dodoma.
Katika mchezo huo uliokuwa na presha kubwa, Simba SC ilionekana kutawala sehemu kubwa ya mchezo kwa kumiliki mpira na kushambulia mara kwa mara lango la Dodoma Jiji. Washambuliaji wa Simba walijaribu kupenya ukuta wa safu ya ulinzi ya wapinzani wao kwa mashambulizi ya kasi kupitia pembeni na katikati ya uwanja, lakini walikosa umakini wa kumalizia nafasi walizozipata.
Dodoma Jiji, licha ya kubanwa kwa muda mrefu, walionesha nidhamu kubwa ya kiulinzi katika kipindi chote cha mchezo huo.
Kipa wa Dodoma Jiji alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kuokoa michomo kadhaa hatari iliyolenga lango lake.
Mashabiki wa Simba walionekana kukata tamaa mara kadhaa kutokana na timu yao kushindwa kutumia vyema nafasi walizotengeneza, hasa katika dakika za mwisho za mchezo ambapo presha ilikuwa kubwa zaidi.
Kwa matokeo hayo, Simba SC inajikuta ikipota alama ugenini katika mbio za ubingwa, huku Dodoma Jiji wakiondoka kifua mbele kwa kupata pointi moja muhimu dhidi ya moja ya vigogo wa soka nchini.
Mchezo huo umeonesha kuwa ushindani katika Ligi Kuu Tanzania Bara unaendelea kuwa mkali, huku kila timu ikipambana kuhakikisha inapata matokeo chanya katika kila mechi.
Simba SC Machi 1, 2026 watakuwa na kibarua kizito kuwakabili watani zao Yanga SC katika mchezo Ligi Kuu Tanzania Bara utakao pigwa Dimba la Amani Complex, Visiwani Zanzibar.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment