Wafanyabiashara wa Soko la Nyama Choma Vingunguti wamefunga maduka yao leo na kuanza mgomo wa baridi wakipinga ongezeko la tozo na ushuru zinazodaiwa kuwakamata kiuchumi.
Soko hilo lilionekana kimya mapema asubuhi, huku milango ya maduka ikifungwa kwa nguvu na wamiliki wa biashara wakiwa wamekaa kwa vikundi wakijadiliana kuhusu hatua za kuchukua. Wafanyabiashara hao walisema tozo za uendeshaji, ukaguzi na ushuru zimekuwa nyingi kupita kiasi, jambo ambalo limewafanya kupoteza faida na kushindwa kulipa madeni ya bidhaa.
“Mara nyingi tunauzwa kwa hasara; tozo ni nyingi na zinatuua kiuchumi,” alisema mfanyabiashara mmoja, akionyesha mfuko wake wa pesa uliokuwa mfupi.
Wafanyabiashara hao walisema mgomo huo ni wa amani na hawana nia ya kuvunja sheria, bali wanataka serikali na mamlaka husika waingie mezani mara moja ili kutafuta suluhisho. “Tunapigana kwa biashara zetu, si kwa vurugu,” alisema mmoja wao.
Hadi saa za mchana, soko lilikuwa kimya na wateja wengi waliokuwa wametegemea kununua nyama kwa sherehe za familia walilazimika kurudi nyumbani bila huduma. Wengine walibaki nje ya soko wakiwa na taharuki, wakihofia maisha yao ya kiuchumi na usalama wa biashara zao.
Mwenyekiti wa soko, Mohamed Mweku maarufu kama Mwarabu, alisema amepokea kadhia hiyo kutoka kwa wafanyabiashara na kuahidi kuwasilisha malalamiko yao kwa mamlaka husika. Aliongeza kuwa soko linakabiliwa pia na changamoto nyingine kama joto na moshi, malipo ya vyoo na ukosefu wa zebra kwa wapita njia barabarani.
Wafanyabiashara wanasema wanatarajia majibu ya haraka kutoka kwa serikali, huku wakiomba tozo ziwe na uwiano na uwezo wa wajasiriamali ili kuepusha kufungwa kwa biashara.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment