" WATENGENEZA MAUDHUI MITANDAONI NA WAANDISHI WA HABARI WANUFAIKA NA PROGRAMU ZA IMBEJU NA GOGLIN YA CRDB FOUNDATION

WATENGENEZA MAUDHUI MITANDAONI NA WAANDISHI WA HABARI WANUFAIKA NA PROGRAMU ZA IMBEJU NA GOGLIN YA CRDB FOUNDATION

Na Mwandishi wetu,  Misalaba Media 

Watengeneza maudhui mitandaoni pamoja na waandishi wa habari nchini wamepata fursa mpya za maendeleo kupitia programu za IMBEJU na GOGLIN zinazoratibiwa na CRDB Bank Foundation, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha vijana na wanawake wa Kitanzania kiuchumi na kitaaluma.

Akizungumza katika shughuli ya IST Festival kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bi. Tuliester Mwambamba, Meneja Muwezeshaji Vijana na Wanawake wa CRDB BankFoundation Bw.Shamiri Kamtu  amesema taasisi hiyo imelenga kuwafikia wabunifu wa maudhui ya kidijitali pamoja na wanahabari ili waweze kunufaika na mafunzo, mitandao ya kitaaluma na fursa za kujikwamua kiuchumi.

Kamtu amesema kupitia udhamini wa tamasha hilo, vijana wengi wameanza kuona mwanga wa mafanikio kwa kupata taarifa na elimu kuhusu namna ya kujiunga na programu hizo ambazo tayari dirisha la maombi limefunguliwa rasmi. Alisisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha vijana wanatumia ubunifu wao kama njia ya kujenga ajira na kuongeza kipato.

Kwa upande wake, mwakilishi wa CRDB Insurance Company, Omary Merere, amesema ushiriki wao kwenye tukio hilo unalenga kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa bima ya magari huku wakitoa huduma hapo kwa hapo ili kurahisisha upatikanaji wa bima kwa wananchi.

Merere amefafanua kuwa licha ya kampuni hiyo kuwa changa sokoni, imejipanga kuimarisha mifumo ya huduma kwa wateja kwa kuhakikisha madai halali yanalipwa kwa wakati na mchakato wake kuwa mfupi, jambo linaloongeza imani kwa wateja.

Aidha, viongozi hao walieleza kuwa uwekezaji katika vijana na wanawake ni msingi wa maendeleo ya taifa, huku programu za IMBEJU na GOGLIN zikitarajiwa kuongeza idadi ya wabunifu na wanahabari watakaonufaika na fursa za kifedha na kitaaluma.

Hatua hiyo imepokelewa kwa matumaini makubwa na washiriki wa tamasha, wengi wakisema ni mwanzo wa safari mpya kwa watengeneza maudhui mitandaoni na waandishi wa habari wanaotafuta nafasi za kupanua kazi zao katika era ya kidijitali.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post