" BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA MUSOMA ROBO YA PILI KUJADILI MAENDELEO YA MANISPAA

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA MUSOMA ROBO YA PILI KUJADILI MAENDELEO YA MANISPAA

 


Machi 6, 2026, Baraza la Madiwani la Manispaa ya Musoma limekutana kwa kikao maalumu cha kupokea na kuchambua ripoti kutoka kwa kamati mbalimbali za baraza. Kikao hiki kililenga kuhakikisha maamuzi yanayofanywa yanasaidia kuendeleza ustawi wa wananchi na maendeleo ya Manispaa kwa jumla.


Meya wa Manispaa, Mheshimiwa Alex Nyabiti, alisisitiza umuhimu wa mjadala wa kina kuhusu taarifa zilizowasilishwa na kamati, ili kila uamuzi uwe na manufaa kwa wananchi na uchumi wa Manispaa.

kamati zilizowasilisha ripoti ni Kamati ya Mipango Miji na Mazingira Kamati ya Fedha

Kamati ya Elimu, Afya na Huduma za Uchumi

Ripoti hizo ziliwasilisha utekelezaji wa majukumu yao ya kipindi kilichopita, huku madiwani wakijadiliana hatua za kuboresha huduma na kuimarisha maendeleo ya Manispaa.


Aidha, Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Mheshimiwa Miraji Mgore Kigera, alishauri Kamati ya Fedha kuongeza juhudi katika kufuatilia wadaiwa wa nyuma, kama ilivyopendekezwa na Serikali ya Mkoa, ili kuongeza mapato na kuboresha huduma kwa wananchi.



Diwani wa Kata ya Rwamlimi, Mheshimiwa Peter Bernard, alisisitiza kuongezwa kwa muda wa leseni za vileo ili kuongeza mapato ya Manispaa. Pia aligusia mpango wa kutoa tuzo kwa kushirikiana na Bongo Buzz, lengo likiwa ni kuhamasisha na kuthamini mchango wa wadau katika maendeleo.


Kikao kilikamilishwa kwa Mwenyekiti wa Baraza kusisitiza utekelezaji wa maagizo yote yaliyotolewa.


Mkurugenzi wa Manispaa amelekezwa kushirikiana na wataalamu wake kuhakikisha ufungaji wa kamera za CCTV kwenye ofisi za Halmashauri kwa ajili ya usalama. Pia, baraza limezingatia usafi wa mazingira na kuagiza ukusanyaji wa taka kufanywa kwa wakati. Hatimaye, ujenzi wa machinjio ya kuku Nyasho umeagizwa kuharakishwa ili kuendeleza huduma na shughuli za kiuchumi kwa wananchi.




 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post