Na mwandishi wetu Misalaba Media
Mbeya
Mapambano ya kuboresha miundombinu ya barabara mkoani Mbeya yanaendelea kushika kasi chini ya usimamizi wa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, ambaye amekuwa mstari wa mbele kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo na kutatua changamoto zinazoikabili.
Akizungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika jijini Mbeya na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa, Beno Malisa, Mhandisi Bishanga alieleza kuwa miongoni mwa changamoto zilizokuwa zikikwamisha maendeleo ni uwepo wa nguzo za umeme katika eneo la Iwambi–Mbalizi ambapo kupitia uratibu kati ya TANROADS na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), hatua za mwisho zinaendelea kuchukuliwa kuondoa nguzo hizo ili kumpa mkandarasi nafasi ya kuendelea na kazi bila vikwazo.
Aliongeza kuwa sehemu ya njia ya mchepuo katika eneo hilo tayari imeanza kutumika kwa kiwango fulani, hatua inayotarajiwa kupunguza msongamano wa magari pamoja na ajali katika eneo hilo muhimu la usafiri.
Kuhusu barabara ya Mbalizi kuelekea Shigamba, Mhandisi Bishanga amesema maandalizi ya ujenzi wa kipande cha kwanza cha lami yamekamilika na mkandarasi tayari amepatikana kwa ajili ya ujenzi wa kilomita 10 za mwanzo.
Aidha Bishanga aliongeza kuwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina unaendelea katika maeneo ya Kimo, huku barabara hiyo ikitajwa kuwa kiunganishi muhimu kuelekea Itumba na Isongole mkoani Songwe.
Katika hatua nyingine, ameainisha kuwa serikali imeagiza maeneo korofi katika barabara ya Isonje–Kikondo, inayounganisha mikoa ya Mbeya na Njombe, yawekwe zege ili kurahisisha safari za wakulima na wasafirishaji wa mazao, hususan kutoka Makete kwenda Mbeya.
Juhudi Meneja huyo zinaonyesha dhamira ya serikali ya kuimarisha mtandao wa barabara mkoani Mbeya kwa lengo la kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuboresha usalama wa watumiaji wa barabara.
Hata hivyo Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Mbeya Beno Malisa aliipongeza Tanroads Kwa juhudi za kutekeleza miradi ya Barabara kwa wakati huku akihimiza viongozi kusikiliza na kutatua kero za wananchi wakati wote.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment