Na Lydia Lugakila-Misalaba Media MbeyaMjasiriamali kutoka mkoani Mbeya anayejishughulisha na uuzaji wa malighafi za kutengenezea sabuni za maji na vipande, mishumaa pamoja na mafuta ya mgando na batiki Bi Colletha Simon Kipeta amewahimiza wanawake mkoani Mbeya kutobweteka bali kujishughulisha na shughuli za kiuchumi ili kuweza kusaidia na kuzipambania familia zao.Bi. Kipeta ametoa wito huo alipotembelea watoto yatima katika Shule ya Sekondari Vanessa yeye pamoja na wanawake wafanyabiashara Mkoani humo ziara waliyoshiriki kutoa msaada pamoja na kuwapa moyo watoto yatima ili waendelee kusoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao.Akizungumza baada ya hafla hiyo, Bi kipeta amesema kuwa wanawake wana nafasi kubwa ya kufanya mabadiliko katika jamii endapo watajituma katika ujasiriamali na kutumia fursa zilizopo kujiongezea kipato.Aidha, amesisitiza kuwa wao kama wanawake wafanyabiashara wataendelea kudumisha utamaduni wa kusaidia na kuwafikia watu wenye uhitaji katika jamii, ikiwemo watoto yatima, ili kuwapa matumaini na kuwafanya wajione kuwa ni sehemu ya jamii inayowajali.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment