" DKT. JINGU AWATAKA WAJASIRIAMALI KUONGEZA UBUNIFU KUFIKIA SOKO LA KIMATAIFA

DKT. JINGU AWATAKA WAJASIRIAMALI KUONGEZA UBUNIFU KUFIKIA SOKO LA KIMATAIFA






Na WMJJWM- Dar Es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu, amewataka wajasiriamali nchini kuongeza ubunifu katika uzalishaji wa bidhaa zao ili kupanua soko na kufikia ushindani katika soko la kimataifa.

‎Dkt Jingu ametoa kauli hiyo, katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam, wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Chemba ya Wanawake Wafanya bishara Tanzania (TWCC). Ameeleza kwamba ni wakati wa wajasiriamali, hususan wanawake, kuzingatia ubora, viwango na ubunifu wa bidhaa ili ziweze kukidhi mahitaji ya masoko ya ndani na nje ya nchi.

‎Dkt Jingu amesisitiza kwamba maenesho hayo ni jukwaa muhimu kwa wajasiriamali kutangaza na kuuza bidhaa zao, kujifunza mbinu bora za biashara na kujenga mtandao mpana wa wateja na wadau wa maendeleo.

‎Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Dkt. Mwajuma Hamza, amesema kuadhimisha Miaka 20 ni ushahidi wa dhamira, uthubutu na mshikamano wa wanawake wajasiriamali nchini ambao wameamua kuinuka, kujikwamua kiuchumi na kuchangia maendeleo ya Taifa.

‎“Katika kipindi hiki chote, taasisi yetu imeendelea kuwa daraja la kuwaunganisha wanawake wajasiriamali na fursa za masoko, mitaji, mafunzo na mitandao ya kibiashara. Tumejenga jukwaa la sauti ya mwanamke mjasiriamali, tukitetea maslahi yao na kushirikiana na serikali pamoja na wadau wa maendeleo kuboresha mazingira ya biashara”. Amesema Dkt. Mwajuma

‎Naye Paula Joseph mjasiriamali aliyeshiriki maonesho hayo, amesema amepata manufaa makubwa kwa kutangaza bidhaa zake na kuongeza wigo wa wateja. Amesema ushiriki wake umefungua milango mipya ya kibiashara na kumpa uzoefu wa kiushindani.

‎Paula amewahimiza wanawake na wasichana kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonesho na maadhimisho kama hayo, akibainisha kuwa ni fursa adhimu ya kuuza bidhaa, kujifunza na kupanua soko.

‎Maadhimisho hayo ni sehemu muhimu kwa wajasiriamali kuonesha uthubutu katika uzalishaji wa bidhaa zao ili kufikia soko la kimataifa na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.

 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post