Na Lydia Lugakila- Misalaba MediaMbeyaRais wa Umoja wa Mabunge Duniani na Mbunge wa Jimbo la Uyole, Mhe. Dkt. Tulia Akson, amempongeza Diwani wa Kata ya Ilemi, Mhe. Baraka Zambi, pamoja na viongozi wote wa kata hiyo kwa juhudi na jitihada wanazozifanya katika kuwatumikia wananchi.Pongezi hizo amezitoa kufuatia hatua ya viongozi hao kuendelea kuandaa mikutano ya hadhara kwa wananchi, kusikiliza kero zao na kushirikiana kutafuta suluhisho.Baadhi ya changamoto zimekuwa zikipatiwa ufumbuzi katika ngazi ya kata, huku zingine zikipelekwa katika ngazi za juu kwa ajili ya kufanyiwa kazi.Katika hatua nyingine, Dkt. Tulia amepokea ombi la mhe Zambi kuhusiana na changamoto ya mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Jiji kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Ameahidi kulifanyia kazi ombi hilo mara moja ili kuhakikisha mikopo hiyo inawafikia walengwa kwa ufanisi.Aidha, amemshauri Afisa Maendeleo wa Kata ya Ilemi kutoa elimu ya kutosha kwa jamii kuhusu mikopo hiyo, ikiwemo taratibu na namna ya kuomba, ili kusaidia kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa mchakato wa uombaji wa mikopo hiyo.Kuhusu miundombinu, Dkt. Tulia amewaahidi wananchi wa kata hiyo kuwa barabara ya Juhudi katika Mtaa wa Masewe, ambayo ipo kwenye mradi wa TARURA, itajengwa ili kuondoa adha wanayopata wananchi wanaoitumia. Pia ameahidi kuzungumza na kumuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya pamoja na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha ujenzi wa barabara za Mwandemange, Dondori na barabara nyingine zenye changamoto katika kata hiyo unatekelezwa ili kuboresha usafiri na usafirishaji kwa wananchi.Hata hivyo, Dkt. Tulia alihitimisha kwa kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa karavati (kivuko) kinachounganisha balozi nne za Mtaa wa Ilinji. Katika mchango huo, ametoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa mifuko 30 ya saruji ili kusaidia kukamilisha ujenzi wa kivuko hicho ambacho kitasaidia kurahisisha mawasiliano na shughuli za wananchi wa eneo hilo.
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani na Mbunge wa Jimbo la Uyole, Mhe. Dkt. Tulia Akson.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment