
Kwa muujibu wa Mwandishi wa Habari kutoka nchini Ghana {@mickyjnrofficial } anaarifu kuwa,
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana anayekipiga ndani ya klabu ya Simba SC, Jonathan Sowah, amevunja ukimya na kutoa majibu ya kina dhidi ya tuhuma mbalimbali za utovu wa nidhamu na uhujumu zilizopelekea kusimamishwa kwake. Sowah amejitokeza kusafisha jina lake, akigusia pointi nane (8) muhimu zinazozua mjadala mzito miongoni mwa mashabiki wa “Wekundu wa Msimbazi.”
Mambo Muhimu Katika Majibu ya Sowah:
1.Kususia Mazoezi: Amekana kugoma kufanya mazoezi mnamo Februari 17 (dhidi ya Greenland FC), akidai alifanya mazoezi ya “activation” licha ya kuwa alikuwa amesimamishwa na asingeruhusiwa kuingia uwanjani.
2. Vifaa vya Mazoezi: Kuhusu tukio la Februari 22, ameeleza kuwa kuchelewa kwake kulisababishwa na changamoto za usafiri na kukosekana kwa vifaa (training kit), lakini baadaye alikamilisha mazoezi hayo hotelini na wenzake chini ya kocha wa viungo, na kuna video inayothibitisha.
3. Kuchelewa Mazoezi (Feb 16): Amekiri kuchelewa kwa takriban dakika tano baada ya kuzidiwa na usingizi kufuatia kikao cha video, lakini alimtaarifu kocha na hakuwa na nia mbaya.
4. Kuhusu Vikao vya Timu: Amekataa katakata tuhuma za kuchelewa kwenye vikao vya timu (Team Meetings).
5. Jezi ya Benfica: Amekanusha kuvaa jezi ya Benfica safarini kuelekea Angola, akisisitiza alikuwa amevaa sare rasmi ya Simba SC na ushahidi upo kwenye kurasa za kijamii za klabu.
6. Faulo “Zisizo za Kawaida”: Kuhusu tuhuma za kucheza madhambi ya makusudi ili apewe kadi, amesema makosa hayo ni ya kawaida katika ushindani wa soka na hakuwa na nia ya kumuumiza mpinzani au kutolewa nje.
7. Tuhuma za Rushwa: Sowah amekanusha vikali uvumi kuwa alipokea fedha kutoka kwa washindani wao, Young Africans (Yanga) au Singida Black Stars. Ameziita tuhuma hizo kuwa ni za uongo na zenye nia ya kumchafulia jina, akiiomba klabu kufanya uchunguzi na kutoa ufafanuzi wa umma.
8. Ahadi kwa Simba: Amesisitiza kuwa bado ana mapenzi na klabu ya Simba na ameiomba klabu kuondoa adhabu yake au kuitisha kikao cha nidhamu haraka ili aweze kurejea uwanjani.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment