Na Lydia Lugakila-Misalaba Media MbeyaKamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga, amehimiza Askari Polisi wa Kike mkoani humo kuzingatia nidhamu na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.Rai hiyo ameitoa Machi 13, 2026, wakati akifungua kikao kazi cha siku moja cha Mtandao wa Polisi wa Kike Mkoa wa Mbeya kilichofanyika katika ukumbi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia.Kamanda Kuzaga amepongeza juhudi na ushirikiano wa mtandao huo katika utekelezaji wa majukumu ya kipolisi kwa kipindi cha mwaka 2025. Pia ameutambua mchango wao katika shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo utoaji wa elimu kwa makundi ya jamii pamoja na ushiriki katika matendo ya huruma kwa watu wenye mahitaji maalum.Aidha, Kamanda Kuzaga amewataka askari hao kuwa chachu ya mabadiliko katika utendaji kazi wa Polisi na kutumia vyema fursa za kujiendeleza kielimu kupitia vyuo vikuu na vyuo vya kati vilivyopo ndani ya Mkoa wa Mbeya.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wa Kike Mkoa wa Mbeya, SSP Salome Kabanje, amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa kipindi cha robo mwaka pamoja na kuweka mikakati mipya ya kuboresha utendaji.Ameongeza kuwa elimu waliyoipata kutoka kwa wawezeshaji itasaidia kuboresha utendaji kazi wao na imewajengea uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya kisaikolojia na mawasiliano baina yao.Naye mmoja wa wawezeshaji kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, ambaye ni mtaalamu wa saikolojia Betuna Mwamboneke, amesema elimu ya saikolojia wanayoitoa kwa jamii inasaidia kuongeza uelewa na kuwahamasisha watu kutafuta tiba mapema wanapokutana na changamoto mbalimbali za afya ya akili.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment