
Na Mary SangaMbeyaKanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Konde, Jimbo la Mbeya Magharibi, limemuaga rasmi aliyekuwa Mkuu wa Jimbo hilo lenye makao makuu Iwambi, jijini Mbeya.Mchungaji Lusajano Sanga ameagwa baada ya kumtumikia Mungu katika Jimbo hilo kwa zaidi ya miaka mitatu.Amehamishiwa kwenda kumtumikia Mungu katika nafasi nyingine ya ukuu wa chuo kinachozalisha watumishi wa Mungu, wakiwemo wainjilisti pamoja na wanafunzi wa kozi nyingine mbalimbali ambopo Chuo hicho kipo katika kijiji cha Matema, wilayani Kyela.Akizungumza katika ibada ya kuagwa rasmi, Mchungaji Sanga ameeleza mafanikio aliyoyapata katika kipindi cha uongozi wake ikiwemo kueneza Injili katika vijiji vya Ifwengenya, na amesisitiza kuwa hilo ndilo agizo kuu walilopewa Wakristo wote na Mungu.Sanjari na hilo, Mchungaji Sanga amesema kuwa kwa kushirikiana na wachungaji wengine walijitahidi pia kuwafikia wananchi kwa kuwapatia mahitaji muhimu ya kibinadamu, ikiwemo nguo.Aidha, ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana katika kipindi chake cha uongozi, likiwemo ujenzi wa msingi wa ofisi bora ya Jimbo hilo.Kwa upande wake, Mkuu wa Jimbo kwa sasa, Nancy Maro, ameahidi kuendelea kushirikiana vyema na wachungaji katika mambo yote ili kuendeleza kazi ya Mungu kwa ubora na ufanisi zaidi, jambo ambalo litaongeza ustawi wa kiroho pamoja na uchumi.Hata hivyo, Mchungaji Benson Mwaijande pamoja na Mchungaji Juliana kwa pamoja wamesema kuwa katika kipindi ambacho Mchungaji Sanga amekuwa kiongozi wao, wamefanya kazi kwa ushirikiano mkubwa katika kuendeleza kazi ya Mungu kwa ubora. Pia wameongeza kuwa Mchungaji Sanga alikuwa kiongozi mnyenyekevu na mtiifu.

Post a Comment