" LORI LATEKETEA KWA MOTO MOROGORO, MTU MMOJA AFARIKI

LORI LATEKETEA KWA MOTO MOROGORO, MTU MMOJA AFARIKI

 Farida Mangube Morogoro

Lori la mizigo lenye namba za usajili T729 BBT pamoja na tela namba T677 BTY limeteketea kwa moto katika eneo la Lugono, karibu na Nyama Choma Barabara Kuu ya Iringa–Morogoro.

Tukio hilo la Lori kuwaka moto limetokea usiku wa kuamkia March 19 katika mazingira ambayo bado hayajafahamika wazi ambapo limeathiri vibaya sehemu ya mbele ya gari hiyo.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuudhibiti moto huo kabla haujasambaa zaidi, licha ya uharibifu mkubwa uliokwisha kutokea 

Fullushangwe Blog imefikia katika eneo na kushuhudia lori hilo likiwa linateketea huku juhudi za uokoaji zikiendelea.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, mtu mmoja anasadikika kupoteza maisha kufuatia tukio hilo. Inadaiwa kuwa mwili wa mtu huyo uliungua vibaya kiasi cha kufanya utambuzi kuwa mgumu, huku mabaki yanayoaminika kuwa ya binadamu yakionekana katika eneo la tukio, ingawa utambuzi rasmi bado unasubiri uthibitisho wa mamlaka husika.

Wakati huo huo, jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro zinaendelea ili kutoa taarifa rasmi kuhusu chanzo cha ajali hiyo, kuthibitisha idadi ya waathirika pamoja na kueleza hatua zinazochukuliwa.    

 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post