Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Mhe. Johnston Mutasingwa, ameendelea kugusa maisha ya wananchi kwa kutoa Mkono wa Idd kwa Kwa Wazee 25 wa Kata ya Kashai, Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera
Msaada huo uliolenga makundi maalum wakiwemo wazee pamoja na wanufaika wa mpango wa TASAF, Ambapo Msaada huo umekabidhiwa rasmi na Katibu wa Mbunge kwa niaba yake, ambapo aliwasilisha salamu na nia njema ya mbunge huyo kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Katibu wa Mbunge alieleza kuwa msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa Mhe. Mutasingwa wa kuwasaidia wananchi wake hususan katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kwa Waislamu, pamoja na kipindi cha mfungo wa Kwaresma kwa Wakristo.
Alibainisha kuwa mbunge huyo amekuwa na utamaduni wa kutoa mkono wa Idd na amesema Kuwa Ataendelea kuwafikia wananchi wenye uhitaji na kuwaletea faraja katika nyakati za ibada na sikukuu.
Baadhi ya wanufaika wa msaada huo walitoa shukrani zao za dhati kwa mbunge huyo, wakisema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka na utawasaidia katika maandalizi ya sikukuu ya Idd.
Kadhalika,Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Ameomba Wananchi wa Jimbo la Bukoba kuendelea kushirikiana kwa karibu na wananchi wa jimbo hilo, huku akiwaomba ushirikiano wa kutosha ili kuendeleza juhudi za maendeleo na ustawi wa jamii nzima.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment