"
NABII MPANJI ASISITIZA UAMINIFU KWA VIONGOZI WA SERIKALI NA WAKRISTO
Mchungaji wa Kanisa la Gospel Miracle Church For All People (GMCL), Nabii na mtumishi wa Mungu David Mpanji, akihubili neno la MunguNa Lydia Lugakila- Misalaba Media MbeyaMchungaji wa Kanisa la Gospel Miracle Church For All People (GMCL), Nabii na mtumishi wa Mungu David Mpanji, amewataka viongozi wa serikali pamoja na wakristo kwa ujumla kujenga tabia ya uaminifu katika maeneo yao ya kazi ili kulijenga taifa lenye neema na baraka za Mungu.Nabii Mpanji ametoa kauli hiyo kupitia ibada iliyofanyika Machi 15, 2026 ambapo amewahimiza Wakristo kuwa waaminifu katika maisha yao ya kila siku akisisitiza kuwa njia pekee ya kuwa rafiki wa Mungu ni kuwa mwaminifu.Akizungumza wakati wa mafundisho yake, Nabii Mpanji amesema viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu na wabunge wanapaswa kuwa waaminifu hasa wanapopewa dhamana ya kusimamia fedha za umma.Mtumishi huyo wa Mungu amesema anamshukuru Mungu kwa kumwona mwaminifu katika huduma yake, kazi ambayo inahitaji kusikiliza kwa makini sauti ya Roho Mtakatifu.Nabii huyo ameeleza kuwa wiki mbili zilizopita alipokea maelekezo kupitia sauti ya Mungu yaliyomtaka aonyeshe uaminifu kwa kutumia kiasi fulani cha fedha katika kazi ya Mungu.“Namshukuru Mungu kwa maelekezo aliyonipa kupitia sauti yake nimetimiza kwa uaminifu na kama nisingefanya hivyo juzi wakati nafundisha wakristo kuhusu uaminifu, ningekwama najipongeza nimetimiza agizo la Mungu la kutumia fedha nilizoelekezwa kufungua kituo cha televisheni kitakachotangaza neno la Mungu,” alisema nabii huyo.Nabii Mpanji amesema watu wengi hushindwa kupanda katika viwango vya juu vya kiroho kwa sababu ya kukosa uaminifu.Amefafanua kuwa uaminifu ni tunda muhimu katika maisha ya kiroho, kwani mtu anaweza kuwa mtakatifu lakini akakosa matunda ya uaminifu.Aidha amesisitiza kuwa uaminifu na usikivu kwa sauti ya Mungu ni mambo muhimu kwa watumishi wa Mungu, akionya kuwa baadhi ya wahubiri wanapofikia viwango vya juu vya kiroho huanza kufanya mambo kwa mapenzi yao badala ya kufuata maelekezo ya Mungu juu ya uaminifu.Katika nasaha zake kwa Wakristo, Nabii Mpanji amewahimiza Wakristo waliokoka kuishi wokovu wa kweli na kuacha tabia za kitoto katika imani.Amesema wapo wakristo ambao wameokoka kwa zaidi ya miaka 24 lakini bado wanaendelea kuwa na tabia zile zile za zamani, hali inayowazuia kukua kiroho.
Post a Comment