" NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKUTANA NA GO PLANT TANZANIA KUANDAA MJADALA WA NISHATI SAFI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKUTANA NA GO PLANT TANZANIA KUANDAA MJADALA WA NISHATI SAFI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI






Dodoma

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amekutana na Mkurugenzi wa Go Plant Tanzania Bw. Emmanuel Likida kwa lengo la kujadili namna ya kushirikiana katika maandalizi ya Mjadala (Debate) wa Clean Cooking Solutions utakaowahusisha wanafunzi wa shule za Sekondari katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma.

Katika kikao hicho, pande zote mbili zimejadili umuhimu wa kuwajengea vijana uelewa wa mapema kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, athari za matumizi ya nishati zisizo safi kwa afya na mazingira, pamoja na fursa zilizopo katika ubunifu na ujasiriamali wa suluhisho za upishi safi.

Mjadala huo unatarajiwa kuwa jukwaa la kielimu na kimkakati la kukuza uelewa, kuchochea fikra bunifu, na kuibua mabalozi vijana wa Nishati Safi katika jamii.

Kikao hicho kimefanyika leo Machi 03,2026 katika Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post