Na Tonny Alphonce-Misalaba MediaKatika kutekeleza Kwa vitendo kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Dunia 2026 Wanawake wa Mtandao wa Polisi Wanamaji Mwanza Kwa kushirikiana na Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) wametoa elimu ya usalama majini Kwa Wanawake naWasichana wa Sweya mkoani Mwanza.Akizungumza na wakazi hao wa Sweya mkufunzi kutoka Chuo Cha Polisi Wanamaji Mwanza PC Neema Msigwa amesema lengo la kutoa elimu ya kujiokoa katika maji Ili makundi yote yaweze kuvuka salama katika kuipambania Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.Amesema mbinu walizowafundisha zitawasaidia Kuwa Salama endapo dhuruba itatokea ziwani.PC Neema amewataka pia wananchi na wavuvi kukumbuka kuvaa Makoti ya Okozi Kila wanapoingia majini Kwa usalama wao Kwa wakati wote watakapo Kuwa ziwani.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake kutoka Chuo Cha Polisi Wanamaji Mwanza ASP Kagemlo Muhula ameitaka Jamii kuhakikisha Wanawake wanapewa haki ya kufanyakazi Ili kufikia Dira ya Maendeleo ya 2050."Wanawake wanatakiwa pia wasifanyiwe vitendo vya Kikatili Ili awe na akili iliyotulia na amani katika kufanya shughuli za kuzalisha na kuleta maendeleo Kwa familia na taifa Kwa ujumla".alisema ASP KAGEMLO Nae afisa mradi msaidizi kutoka EMEDO Happiness Felix amewataka Wanawake wachakataji wa Sweya kuzingatia usalama wao Kwa Kuwa yoyote anayekuwa karibu na Maji yupo kwenye hatariChuo Cha Polisi Wanamaji Mwanza na Shirika la EMEDO wameshirikiana kutoa elimu ya usalama majini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kuzuia Kuzama Maji Ziwa Victoria unaofadhiliwa na Shirika la Uokoaji Majini (RNLI) Kutoka Uingereza,Isle Of Man na Irish Aid kutoka Ireland.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment