
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amethibitisha kuwa Marekani (US) na washirika wake wa Mashariki ya Kati wamemwomba Ukraine msaada na utaalamu wake wa kivita ili kukabiliana na drones za kujiua za Iran zinazoitwa “Shahed”.
Katika hotuba yake ya jioni (evening address) na mahojiano mengine ya hivi karibuni, Zelenskyy alisema: “Washirika wanageukia kwetu, kwa Ukraine, kwa msaada wa ulinzi dhidi ya ‘Shaheds’ – kwa utaalamu na msaada wa vitendo.
Maombi kuhusu hili yamekuja pia kutoka upande wa Marekani.”Ukraine imepata uzoefu mkubwa wa miaka mingi wa kukabiliana na drones hizi hizo (Shahed), ambazo Urusi imezitumia kwa wingi dhidi ya miji na miundombinu ya Ukraine tangu 2022.
Sasa, baada ya mgogoro wa hivi karibuni kati ya Marekani/Israel na Iran (ambapo Iran imerusha maelfu ya drones na missiles dhidi ya nchi za Ghuba kama UAE, Qatar na Saudi Arabia), Marekani na nchi nyingine zinahitaji maarifa hayo ya Ukraine.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment