Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Mafunzo ya Uanagenzi Awamu ya Nane kwa mwaka 2025/2026 Machi 3, 2026 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Bi.Zuhura Yunus akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya awamu ya nane kwa mwaka 2025/2026 yanayofanyika Chuo cha Ufundi Don Bosco Dodoma Machi 3, 2026.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu akipata maelezo kutoka kwa vijana wa Uanagenzi mara baada ya kutembelea Karakana kabla ya kuanza kwa Hafla ya Uzinduzi wa Mafunzo ya Uanagenzi Awamu ya Nane kwa Mwaka 2025/2026 Machi 3, 2026 Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu wa katikati; kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu,Bi. Zuhura Yunus na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mafunzo ya Uanagenzi Awamu ya Nane kwa mwaka 2025/2026 Machi 3, 2026 jijini Dodoma.Na. Meleka Kulwa- Fullshangwe Blog, Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu amewataka vijana kutumia fursa wanazozipata kuonesha uwezo wao ili waweze kujiajiri, kuajiriwa na hata kuajiri vijana wenzao katika kipindi hiki cha mapinduzi ya teknolojia.
Amesema kuwa vijana wanapaswa kuelewa na kuitumia akili unde (Artificial Intelligence) kwa kuwa si jambo la baadaye bali ni sehemu ya sasa ya mazingira ya kazi, huku akisisitiza kuwa mafunzo wanayopata lazima yaendane na teknolojia ya sasa ya TEHAMA na matumizi ya mifumo ya kidigitali.
Aidha amebainisha kuwa teknolojia si tishio kwa aliye na ujuzi na maadili bali ni fursa kwa aliye tayari kujifunza na kubadilika, akieleza kuwa kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kunahitaji nguvukazi mahiri yenye uwezo wa kuhimili mabadiliko na kushindana katika masoko ya ndani na kimataifa.
Waziri Sangu ameyasema hayo Machi 3, 2026 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya uanagenzi awamu ya 8 kwa mwaka 2025/2026 yanayofanyika Chuo cha Ufundi Don Bosco , ambapo alizitaka taasisi zilizopata nafasi kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanaendana na mahitaji ya soko la ajira.
Katika hatua nyingine amesema kuwa ndani ya miezi 3 zaidi ya vijana 5,000 wamepata fursa za ajira nje ya nchi, huku vijana 1,150 wakitarajiwa kuondoka hivi karibuni kufanya kazi ikiwemo katika kada za udereva na ufundi mitambo, na kuongeza kuwa Serikali inalenga kuona zaidi ya vijana 6,000 wakipata fursa za ajira nje ya nchi katika kipindi hicho.
Aidha amebainisha kuwa Serikali imeanzisha programu maalum ya kuongeza ujuzi kwa nguvukazi hususan wenye ujuzi wa chini ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa taifa, na kwamba lengo ni kufikia mwaka 2050 taifa liwe na nguvukazi yenye ujuzi unaoakisi uchumi wa kipato cha kati ngazi ya juu unaoongozwa na maarifa na maendeleo ya viwanda.
Amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano inaendelea kutekeleza programu ya kukuza ujuzi kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Ameongeza kuwa Serikali imewezesha vijana 5,706 kupitia vyuo 6 vilivyokidhi vigezo, ambapo kati yao vijana wa kiume ni 3,355 na wa kike 2,351, huku jumla ya Sh bilioni 4.3 zikitengwa kwa ajili ya utekelezaji wa programu hiyo.
Aidha amebainisha kuwa wanagenzi 480 wa Mkoa wa Dodoma wamepata ufadhili wa asilimia 100 kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwataka washiriki kuonesha nidhamu, bidii, ubunifu na uadilifu ili mafanikio yao yawe chachu ya maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake, akimuwakilisha Katibu mkuu wa Wizara , Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Bi. Zuhura Yunus amesema kuwa lengo la uzinduzi huo ni kutangaza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi, kuhamasisha vijana kushiriki mafunzo na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo katika kukuza ajira na uchumi.
Aidha, amebainisha kuwa programu hiyo ilianza mwaka 2016/2017 kwa lengo la kuongeza ujuzi wa nguvukazi katika soko la ajira na hadi Februari 2026 jumla ya wanufaika 168,657 wamenufaika.
Awali Akizungumza ,Mkuu wa Chuo cha Don Bosco Vocational Training Centre Dodoma, Mhandisi Dkt. Justin Mulebya amesema kuwa chuo hicho hutoa mafunzo ya ufundi stadi na ufundi sanifu kuanzia ngazi ya 1 hadi ngazi ya 6 (Diploma). pia ameongeza kuwa kwa mwaka huu 2026 chuo hicho kina jumla ya wanafunzi 650, ambapo kati yao wanagenzi 235 wanafadhiliwa na Serikali, wakiwemo wasichana 74 sawa na 31.5% na wavulana 161 sawa na 68.5%
Kauli mbiu ya uzinduzi huo ni “NGUVU KAZI YENYE UJUZI STAHIKI KWA AJIRA ENDELEVU”
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Bi. Alana Nchimbi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya awamu ya nane kwa mwaka 2025/2026 yanayofanyika Chuo cha Ufundi Don Bosco Dodoma Machi 3, 2026.
Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa wa mafunzo ya awamu ya nane kwa mwaka 2025/2026 yanayofanyika Chuo cha Ufundi Don Bosco Dodoma Machi 3, 2026.
Baadhi ya vijana wa Uanagenzi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu alipokuwa akizungumza katika Hafla ya Uzinduzi wa Mafunzo ya Uanagenzi Awamu ya Nane kwa mwaka 2025/2026 Machi 3, 2026 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu alipokuwa akizungumza katika Hafla ya Uzinduzi wa Mafunzo ya Uanagenzi Awamu ya Nane kwa mwaka 2025/2026 Machi 3, 2026 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu alipokuwa akizungumza katika Hafla ya Uzinduzi wa Mafunzo ya Uanagenzi Awamu ya Nane kwa mwaka 2025/2026 Machi 3, 2026 jijini Dodoma.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment