" SERIKALI YAJENGA KITUO CHA MWITIKIO WA HARAKA KUKABILIANA NA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU SONGWE

SERIKALI YAJENGA KITUO CHA MWITIKIO WA HARAKA KUKABILIANA NA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU SONGWE

Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaSerikali imeendelea na juhudi madhubuti za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu ili kuhakikisha ustawi na usalama wa wananchi unaimarika, hususan katika vijiji vinavyopakana na maeneo yaliyohifadhiwa.Katika kuendeleza azma hiyo, Serikali imejenga kituo mahususi cha mwitikio wa haraka katika Kijiji cha Guac, Mkoani Songwe, kwa lengo la kukabiliana na matukio ya wanyama wakali na waharibifu, wakiwamo tembo wanaoingia katika makazi ya watu.Akizungumza mara baada ya kukagua kituo hicho, Afisa Wanyamapori Mkuu, Kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Julius Kimaro, amesema Serikali imeendelea kuimarisha usalama wa watu na mali zao katika vijiji vilivyo jirani na  maeneo yaliyohifadhiwa kwa kujenga vituo vya askari wa wanyamapori vya mwitikio wa haraka.Amesema mbali na ujenzi wa vituo hivyo katika maeneo mbalimbali nchini, Serikali pia imechukua hatua nyingine, ikiwamo uchimbaji wa mabwawa ndani ya hifadhi ili wanyamapori wapate maji bila kulazimika kutoka nje ya maeneo yao ya asili.Aidha, amebainisha kuwa Serikali imekuwa ikijenga vizimba katika mito na maziwa ili kuwalinda wananchi dhidi ya mamba, pamoja na kutumia teknolojia ya ndege nyuki (drone) kufuatilia mienendo ya wanyamapori. Hatua nyingine ni uwekaji wa uzio wa mizinga ya nyuki na uzio wa umeme, ambayo imeendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo hatarishi.“Hivyo, kuwepo hapa ni sehemu ya mwendelezo wa ukaguzi na uimarishaji wa vituo vilivyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuwalinda wananchi na mali zao ili waendelee kuishi kwa amani na furaha,” amesema Kimaro.Awali, Askari Wanyamapori wa Kijiji (VGS), Jeremia Konyembe, ameishukuru Serikali kwa uamuzi wa kujenga kituo hicho, akisema kitasaidia kurahisisha utendaji wa kazi ya kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu.“Tunaipongeza Wizara na  Mhe.Dkt.  Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutujengea kituo hiki. Kazi yetu ya kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu sasa itakuwa rahisi zaidi,” amesema Konyembe

  

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post