Na Gabon Mariba, Musoma Mara.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mara imeandaa iftar maalum ili kuwakutanisha wadau wa mapambano dhidi ya rushwa mkoani humo.
Hafla hiyo, iliyofanyika tarehe 18 Machi, 2026 katika ukumbi wa MK Hotel, Musoma Mjini, ulifurika kwa viongozi na wananchi waliokusanyika kwa iftar ya pamoja iliyoratibiwa na TAKUKURU Mkoa wa Mara.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, wazee maarufu, Kamati ya amani na maridhiano ya Mkoa wa Mara, watumishi wa serikali, wakuu wa idara, watu wenye mahitaji maalum, mashekhe, maafisa usafirishaji(Bodaboda na Bajaji) ,Skauti pamoja na wafanyakazi wa TAKUKURU Mkoa wa Mara.
Viongozi walisisitiza umuhimu wa kuendeleza na kutunza taifa kwa maslahi mapana ya nchi. Askofu Daniel Ouma aliwashukuru wote, akieleza kuwa umoja huo ni ishara ya upendo na uthibitisho kwamba Watanzania wapo pamoja .
Kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi, Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mhe.Dkt. KHalfan Haule alileta salamu za serikali na kuwataka watumishi wa TAKUKURU kuendeleza moyo huo wa upendo kwa wananchi.
Akizungumza, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara, Simon Ngoma, alisema TAKUKURU ni sehemu ya jamii, hivyo ni wajibu wa taasisi hiyo kuwa karibu na wananchi na kudumisha upendo.
Aidha, Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw. Msabaha Kassim aliipongeza TAKUKURU na kuomba jitihada hizi ziwe endelevu.
Matumizi ya namba 113 ya simu ya bure yalielezwa kama njia muhimu ya kupunguza vitendo vya rushwa na kuhamasisha uwajibikaji katika jamii.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

















Post a Comment