Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika tarehe 08 Machi kila mwaka,Wakala wa huduma za Misitu (TFS) imepokea tuzo ya Shukrani kufuatia udhamini katika hafla ya The citizen rising woman Gala iliyofanyika tarehe 6 Machi Jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa The Super dome.
Tuzo hiyo ambayo ni ishara ya kutambua mchango wa TFS katika kufanikisha hafla hiyo yenye lengo la kutambua na kuthamini mchango wa mwanamke ambao ni chachu katika kuleta maendeleo endelevu nchini imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali za Misitu TFS Dkt. Zainabu Shabani Bungwa.
Pamoja na wadau mbali mbali wanawake kutoka TFS ni miongoni mwa washiriki waliohudhuria hafla hiyo iliyopabwa na midahalo na burudani.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment