
Na. Meleka Kulwa- Fullshangwe Blog, Dodoma
Kupitia Tume ya Madini, Serikali imeendelea kutoa kipaumbele kwa Vijana ambapo hadi kufikia mwezi Desemba 2025, Tume ya Madini imewezesha vijana 2,550 kupata ajira za moja kwa moja kupitia mradi huo. pia katika utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo ambapo katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Desemba 2025, Serikali imetoa jumla ya leseni 5,983 sawa na asilimia 71 ya leseni zote zilizotolewa kwa kipindi husika. Leseni za uchimbaji mdogo wa madini hutolewa kwa Watanzania peke yake ambao sehemu kubwa zimeombwa na kundi la vijana kati ya umri wa miaka 18 hadi 45.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Machi 16, 2026 kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Mhandisi Hamisi Kamando amesema kuwa Tume ya Madini imeendelea kuhakikisha inaongeza ushiriki wa vijana katika shughuli za utunzaji, utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini.
Aidha amebainisha kuwa katika kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2025, Tume ya Madini kupitia mradi wa Mageuzi ya Sekta ya Madini kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu (For Better Tomorrow) imetoa leseni 273 kwa vijana kupitia vikundi vya vijana ambavyo husajiliwa kwenye halmashauri zao.
Pia ameongeza kuwa leseni hizo zilitolewa katika mikoa ya kimadini ya Mara, Mbogwe, Kagera, Shinyanga, Morogoro, Rukwa, Dodoma, Mtwara, Singida, Njombe na Mererani. Leseni hizo zinajumuisha uchimbaji wa madini ya dhahabu, shaba, madini ya vito, madini ya viwandani kama vile chumvi pamoja na madini ya ujenzi.Aidha amebainisha kuwa Tume ya Madini kupitia Wizara ya Madini imeendelea kuweka mazingira ya kisera na kisheria pamoja na kuyasimamia ipasavyo kwa kuhakikisha madini ghafi yanayozalishwa nchini yanaongezwa thamani hapahapa nchini kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
Pia ameongeza kuwa hadi sasa kuna jumla ya viwanda vya usafishaji wa madini (refinery) saba vinavyofanya kazi, huku uongezaji wa thamani wa madini nchini ukizalisha ajira 273, ambapo sehemu kubwa ya ajira hizo ni kwa vijana.Kamando amesema kuwa katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2025 jumla ya madini yenye thamani ya shilingi trilioni 5.8 yaliongezwa thamani nchini.
Aidha amebainisha kuwa Tume ya Madini kwa kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Kituo cha Jemolojia Tanzania (Tanzania Gemological Centre) imeendelea kutoa mafunzo ya uongezaji ujuzi kwa wachimbaji hasa vijana katika maeneo ya uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani pamoja na biashara ya madini.Pia ameongeza kuwa Tume ya Madini kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi Nchini (ACP Skills Program) ilitoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo 579 wanaohusika na umiliki wa leseni, maduara, mialo pamoja na wafanyabiashara wa madini katika mikoa ya kimadini ya Geita, Mbogwe na Chunya.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment