" WANAWAKE RUVUMA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA SAMIA ARDHI KLINIKI KUMILIKI ARDHI

WANAWAKE RUVUMA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA SAMIA ARDHI KLINIKI KUMILIKI ARDHI

Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaWanawake wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya umiliki wa ardhi kupitia kampeni ya Samia Ardhi Kliniki, iliyoanzishwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kampeni hiyo maalum imezinduliwa kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ikiwa na lengo la kutoa elimu na kurahisisha umilikishaji wa ardhi kwa wanawake.Zoezi hilo limeanza rasmi leo Machi 2 na linatarajiwa kuendelea hadi Machi 7 katika Kata ya Peramiho, Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma. Wanawake wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kutumia fursa hiyo muhimu ya kumiliki ardhi kihalali kupitia huduma zinazotolewa katika kampeni ya Samia Ardhi Kliniki.Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Ruvuma, Said Juma Kijiji, amesema lengo kuu la kampeni hiyo ni kuwafikia akina mama wenye changamoto mbalimbali zinazohusiana na masuala ya ardhi, ikiwemo migogoro ya ardhi na upatikanaji wa hati. Amesema kupitia kliniki hiyo, elimu inatolewa ili kuwawezesha wanawake kuelewa haki zao na taratibu sahihi za umilikishaji.Aidha, amewahimiza wanawake kujitokeza kwa wingi kwani kiwanja kilichopimwa lakini hakijamilikishwa kinaweza kuwa chanzo cha migogoro ya baadaye. Amesisitiza kuwa umilikishaji rasmi unatoa usalama wa kisheria na kulinda maslahi ya mmiliki dhidi ya changamoto zinazoweza kujitokeza.Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Ardhi – Mapato na Uwekezaji, Leonard Melchior Msafiri, amesema zoezi hilo ni wito wa wizara unaotekelezwa nchi nzima katika mikoa yote. Ameeleza kuwa ingawa kampeni hiyo imelenga zaidi kuwapa kipaumbele wanawake, wanaume watakaofika watapatiwa huduma kama kawaida, huku akisisitiza umuhimu kwa akina mama kufuatilia matangazo na kujitokeza katika maeneo husika kupata huduma

  

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post