" WAPANDA BASKELI WAKUMBUSHWA KUVUKA ZEBRA KWA KUSUKUMA BASKELI

WAPANDA BASKELI WAKUMBUSHWA KUVUKA ZEBRA KWA KUSUKUMA BASKELI

Wapanda baiskeli katika Manispaa ya Shinyanga wamepewa elimu ya usalama barabarani kuhusu umuhimu wa kuvuka kwa usalama wanapotumia kivuko cha watembea kwa miguu (zebra crossing).


Akitoa elimu hiyo, Sajenti David Ndimila wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga amesisitiza kuwa waendesha baiskeli wanapaswa kushuka na kusukuma baiskeli zao wanapovuka barabara kupitia zebra crossing, kwani kivuko hicho kimetengwa mahsusi kwa watembea kwa miguu.

Ameongeza kuwa kutofuata utaratibu huo kunaweza kusababisha ajali na kuhatarisha usalama wao pamoja na watumiaji wengine wa barabara.

  

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post