Na Lydia Lugakila- Misalaba MediaBukobaWazazi na walezi mkoani Kagera wametakiwa kuwa na mahusiano mazuri na watoto wao ili kujenga kizazi kijacho kilicho bora katika jamii ya Kitanzania.Hayo yamesemwa na Jovith Paschale ambaye ni mhudumu wa Kituo cha Tumaini Children Center kilichopo kata ya Kyakailabwa, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi. Paschale aliyasema hayo wakati wa semina ya kuwajengea uwezo viongozi mbalimbali wa Kata ya Kemondo iliyopo Wilayani Bukoba, ambapo aliwataka wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema ikiwemo kumtumainia Mwenyezi Mungu.Semina hiyo ilifanyika Machi 5 2026 katika ukumbi wa Shule ya Msingi Mbembe na ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo madiwani wa Viti Maalumu, watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji, Mratibu wa Elimu Kata, viongozi wa dini pamoja na viongozi wengine.Lengo la semina hiyo lilikuwa ni kuwajengea uwezo kuhusu ulinzi na usalama wa mtoto katika jamii.Bw. Jovith alisema viongozi hao hawapaswi kukubali kuona mtoto ananyanyasika au kufanyiwa ukatili, bali wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kusambaza elimu waliyoipata ili kusaidia jamii inayowazunguka.“Tuhakikishe watoto wetu wanapata malezi bora kama inavyotakiwa ili baadaye tuwe na kizazi kilicho bora. Hata kama mtoto si wako, kumbuka kuwa mtoto wa mwenzako pia ni wako,” alisema muhudumu huyo.Kwa upande wake, Diwani wa Viti Maalumu kutoka Kata ya Kemondo, Mheshimiwa Zainabu Shakiru, aliwataka viongozi kutumia vyema semina waliyoipata kwa kuisambaza kwa wananchi kupitia mikutano mbalimbali ya kijamii ili elimu ya ulinzi na usalama wa mtoto iwafikie watu wengi kwa haraka.Naye Mtendaji wa Kata ya Kemondo, Cyriacus Sosthenes, alisema wananchi wa Kemondo wanapaswa kushirikiana na serikali pale wanapoona kuna jambo lisilo sahihi linalomhusu mtoto.Hata hivyo alimalizia kwa kutoa onyo kali kwa wazazi na walezi wanaowanyanyasa au kuwafanyia ukatili watoto, akisema kuwa mtu yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria mara moja bila kujali cheo au nafasi aliyonayo.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment