Msanii wa muziki wa Bongo Fleva 20 Percent amefunguka baada ya kuitwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), akieleza kuwa amepokea maelekezo mbalimbali kuhusu kazi zake, ikiwemo wimbo wake mpya Barua. Msanii huyo amesema kikao hicho kilikuwa na lengo la kujenga na kumpa mwelekeo sahihi katika kazi yake ya sanaa, akisisitiza kuwa ameyachukua maelekezo hayo kwa uzito.
Aidha, 20 Percent ameishukuru BASATA kwa kumuita kwa
nia njema, akibainisha kuwa hatua hiyo imempa nguvu mpya ya kurejea kwenye
muziki baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu. Amesema kwa sasa amejipanga kuachia
kazi mpya mara kwa mara, huku akiwaahidi mashabiki wake burudani bora na yenye
ubunifu zaidi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment