Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Steven
Chinyongolo, amesisitiza umuhimu wa malezi ya kiroho kwa watoto na vijana
akieleza kuwa ni msingi muhimu katika kujenga jamii yenye amani, maadili na
mshikamano.
Akizungumza katika uzinduzi wa mtaala wa Mama wa
Upendo pamoja na program ya Alpha uliofanyika katika Klasta ya Shinyanga,
Askofu Chinyongolo amewataka vijana kutumia fursa hiyo kujijenga kiroho na kuwa
na hofu ya Mungu ili waweze kuepuka mienendo isiyofaa inayoweza kuhatarisha
amani ya jamii.
Kwa upande wake, Mwezeshaji wa Klasta ya Shinyanga na
Kahama, Bwana Remi Dumbi, amesema kuwa mtaala huo unalenga kuwawezesha wamama
wa upendo kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika kuwalea na kuwaombea
watoto pamoja na vijana, akibainisha kuwa maombi ni nguzo muhimu katika kujenga
kizazi chenye maadili na kinacholinda amani.
Naye Mchungaji Odras amewahimiza washiriki kumtumaini
Mungu na kuomba uongozi wake katika utekelezaji wa mtaala huo, akisisitiza kuwa
malezi ya kiroho yana mchango mkubwa katika kuimarisha utulivu na amani katika
jamii.
Wakati huo huo, wamama wa upendo wa huduma ya Esta
Encounter katika Klasta ya Shinyanga wameeleza kuwa wameendelea kushirikiana
kwa karibu katika kuwalea na kuwaombea watoto na vijana, wakiamini kuwa kupitia
umoja na mshikamano, wataweza kujenga kizazi chenye maadili kitakachodumisha
amani ya taifa.
Huduma hiyo, iliyoanzishwa mwaka 2008, inalenga kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto na vijana kupitia maombi, ushauri na malezi ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kujenga jamii yenye maadili na amani endelevu.

Mchungaji Odras Gunda
Bwana REMI DUMBI Mwezeshaji wa klasta ya Shinyanga na Kahama
Askofu Steven Chinyongolo. Askofu wa anglican church of Tanzania 
Afisa ustawi wa jamii wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Lydia Kwesigabo akizungumza.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment