" Chatanda ampongeza Rais Samia kutunukuwa PhD ya heshima Chuo cha Nigeria

Chatanda ampongeza Rais Samia kutunukuwa PhD ya heshima Chuo cha Nigeria

Na; Mwandishi Wetu, Dodoma

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC), Mary Chatanda, amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kufuatia kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa cha nchini Nigeria Aprili 11, 2026.

Chatanda ametoa pongezi hizo Aprili 12, 2026, ambapo ameeleza kuwa kazi nzuri za maendeleo zinazofanywa na Rais Dk. Samia katika kustawisha maisha ya wananchi zinatambuliwa si tu Tanzania bali ulimwenguni mwote.

"Heshima aliyoipata Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ni kutokana na kuwa kinara wa nishati safi ya kupikia, afya ya mama na mtoto, taswira nzuri katika masuala ya uongozi kwa wanawake Afrika. Pia Chuo hicho limetambua namna Rais wetu anavyosimamia masuala ya biashara hususani kwa vijana wa Afrika," amesema Chatanda.

Katika hatua nyingine, Chatanda amesisitiza kuwa uongozi mzuri wa Rais Dk. Samia umesaidia kukuza maendeleo nchini na wengi wanajifunza uongozi kupitia yeye (role model).

Ikumbukwe kuwa Chuo hicho kimemtunuku Shahada ya Heshima kama njia ya kutambua mchango wa Rais Dk. Samia katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi, uongozi bora na ustawi wa wananchi.

Kimsingi, hadi sasa, Rais Dk. Samia ameshatunukiwa Shahada saba za Heshima kutoka vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya Tanzania kutokana na kazi nzuri katika kuchochea maendeleo na ustawi wa wananchi.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post