Na Lydia Lugakila-Misalaba Media Mbeya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imeweka rekodi mpya katika sekta ya afya baada ya kupokea zaidi ya shilingi milioni 260 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Matwiga. Hatua hii imeibua mshangao kwa wengi, ikizingatiwa kuwa kwa kawaida Serikali imekuwa ikitoa takribani shilingi milioni 50 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati nchini.Akizungumza na wananchi wa Matwiga Aprili 15 2026, katika siku ya pili ya ziara ya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mhe. Kelvin Nshinshi, amewahimiza wananchi kutumia fursa hiyo kujenga zahanati ya mfano itakayodumisha hadhi ya Chunya kama wilaya ya kuigwa.“Naombeni mtoe ushirikiano katika ujenzi wa mradi huu ili mpate zahanati ya kihistoria hata ninyi mnaona jengo lenyewe ni kubwa na lina utofauti na majengo mengine ya zahanati ambazo Serikali imekuwa ikizijenga,” alisema Mhe. Nshinshi.Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya, Ndugu Anakleth Michombero, amesema utekelezaji wa mradi huo ni ishara ya dhamira ya dhati ya uongozi katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Matwiga na maeneo ya jirani.Ameongeza kuwa ushirikiano wa wananchi utakuwa chachu muhimu katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyokusudiwa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment