" RAIS SAMIA APOKEA UJUMBE WA JUMUIYA YA MADOLA IKULU, DAR ES SALAAM

RAIS SAMIA APOKEA UJUMBE WA JUMUIYA YA MADOLA IKULU, DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Bi. Shirley Ayorkor Botchwey. amesisitiza dhamira ya Jumuiya ya Madola kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha misingi ya demokrasia, utawala bora na maridhiano ya kitaifa. Aidha amesema kuwa Jumuiya hiyo inaunga mkono juhudi zinazoendelea nchini na iko tayari kusaidia kujenga mazingira ya kisiasa yenye utulivu, ushirikishwaji na kuaminiana kupitia mazungumzo na mageuzi ya taasisi.Hayo yamo katika ujumbe wake uliowasilishwa na Mjumbe Maalum na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Ikulu ya Dar es Salaam, leo.Jumuiya ya Madola imesema kwamba inafuatilia kwa makini matukio yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ikiktaka kushiriki kwa uwazi katika juhudi za kuendeleza majadiliano ya vyama na kuimarisha uwajibikaji wa taasisi.Akizungumza wakati wa kupokea ujumbe huo, Rais Dkt. Samia amesema Tanzania inaendelea kushughulikia hali hiyo kupitia taasisi zake, akizitaja hatua zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo kuunda Tume Huru ya Uchunguzi kwa lengo la kurejesha utulivu na kuimarisha uwajibikaji. Amebainisha kuwa matokeo ya Tume hiyo yataongoza hatua zinazofuata ikiwemo uwajibikaji, maridhiano na mageuzi ya taasisi, huku Serikali ikiendelea kusimamia mchakato wa maridhiano kupitia majukwaa ya kisheria na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali.Kwa upande wake, Mhe. Chakwera ameeleza utayari wa Jumuiya ya Madola kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha utawala wa sheria na mshikamano wa kitaifa. Dkt. Chakwera amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini baada ya kufanya tathmini ya hali ya kisiasa na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa kisiasa na kitaasisi nchini.______________PRESIDENT SAMIA RECEIVES COMMONWEALTH MESSAGE AT DAR ES SALAAM STATE HOUSECommonwealth Secretary-General Shirley Ayorkor Botchwey has reaffirmed the Commonwealth's commitment to continued engagement with Tanzania in reinforcing democratic governance, the rule of law, and national reconciliation. Furthermore, she stated that the Commonwealth supports ongoing efforts in the country and stands ready to assist in fostering a stable, inclusive, and credible political environment through dialogue and institutional reforms.This was contained in a special message delivered by Special Envoy and former President of the Republic of Malawi, His Excellency Dr. Lazarus McCarthy Chakwera, to the President of the United Republic of Tanzania, Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, at the Dar es Salaam State House today. The Commonwealth noted that it is closely monitoring developments during and after the October 2025 General Election, seeking transparency and cooperation in advancing inter-party dialogue and strengthening institutional accountability.Speaking while receiving the message, President Samia stated that Tanzania is addressing the situation through its national institutions, citing measures undertaken by the Government including the establishment of an independent Commission of Inquiry aimed at restoring stability and enhancing accountability. She noted that the findings of the commission will inform subsequent actions, including accountability processes, reconciliation efforts, and institutional reforms, while the Government continues to facilitate dialogue through legally established platforms and broad stakeholder engagement.For his part, Dr. Chakwera reiterated the Commonwealth's readiness to work with Tanzania in advancing the rule of law and national cohesion. Dr. Chakwera concluded his working visit to the country after assessing the political environment and holding consultations with a range of political and institutional stakeholder

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post