" DEREVA WA GARI LA KAMPUNI YA JAMBO AUAWA KIKATILI MKOANI SINGIDA

DEREVA WA GARI LA KAMPUNI YA JAMBO AUAWA KIKATILI MKOANI SINGIDA



Na Saulo Stephen – Singida.

Dereva wa gari la Kampuni ya Jambo Food Product yenye makao makuu yake Mkoani Shinyanga aliyefahamika kwa jina la James Sanga Nkwabi (57), Mkaazi wa Nzega Mkoani Tabora, amekutwa ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye nkali shingoni na watu wasiofahamika, katika kitongoji cha unyambwa kilichopo kijiji cha Mkiwa kata ya Mkiwa, wilaya ya Ikungi Mkoani Singida. Marehemu James Sanga Nkwabi.

Akizungumza na jambo Media Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Amon Kakwale, amesema tukio hilo limetokea tarehe 26 2026, majira ya saa 11 alfajiri katika kitongoji cha Unyambwa Kilichopo Kijiji na Kata ya Mkiwa Wilayani Ikungi Mkoani Singida ambapo marehemu alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 717 DZW na teller namba T 740 DZL mali ya Kampuni ya Jambo food Product ya Shinyanga.

Aidha Kamanda Kakwale ameongeza kuwa dereva huyo alikuwa akitokea Dar es Salaam kwenda shinyanga ambapo mwili wa James ulikutwa hatua 50 kutoka kwenye gari alilokuwa akiendesha. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Amon Kakwale.

Hata hivyo chanzo cha tukio bado hakijafahamika ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi, ili kubaini dereve huyo alikuwa nani mpaka kifo kinatokea ambapo uchunguzi wa awali ulionesha ndani ya gari kulikutwa kisu.

Kamanda Kakwale ametoa wito kwa madereva hususani wa magari makubwa, ambayo hayaruhusiwi kupakia abiria kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani kwa kuwapa rift au kubeba watu wasiowafahamu.

Taarifa ya Kamanda huyo imeeleza kuwa, vitu vyote vya marehemu vimekutwa vipo na hakuna upotevu wowote wa mali zilizobebwa ndani ya gari hiyo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post