Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Dk Juma zuberi Homera Aprili 11, 2026, Amekabidhi rasmi magari mawili kwa Ofisi ya TANESCO wilayani Namtumbo, hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kasi ya utoaji wa huduma ya umeme katika jimbo letu.Kupatikana kwa magari haya ni sehemu ya juhudi endelevu za kuboresha miundombinu na kuimarisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi, hususan katika maeneo ya vijijini na pembezoni. Magari hayo yanatarajiwa kurahisisha shughuli za kiutendaji, ikiwemo usimamizi wa miradi ya umeme, matengenezo ya miundombinu, pamoja na kushughulikia changamoto za huduma kwa wakati.Aidha Mh Mbunge Amepongeza TANESCO kwa jitihada zake madhubuti katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme kwa uhakika, hatua ambayo inaendelea kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo mbalimbali."Ninawapongeza watumishi wa taasisi hiyo kwa kujituma kwao na kuwasihi kuyatunza vyema magari hayo ili yaweze kudumu na kutoa tija iliyokusudiwa. Matumizi sahihi ya rasilimali hizi ni muhimu katika kufanikisha azma ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi"
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment