" Waziri Nyansaho Aongoza Harambee, Milioni 641 Zakusanywa Ujenzi wa Ofisi ya SDA North Mara

Waziri Nyansaho Aongoza Harambee, Milioni 641 Zakusanywa Ujenzi wa Ofisi ya SDA North Mara



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Ryimo Nyansaho, ameongoza harambee iliyofanikiwa kukusanya jumla ya shilingi milioni 641 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) katika Jimbo jipya la North Mara Field.

Katika harambee hiyo iliyofanyika Aprili 11, 2026 katika Kanisa la SDA Kibumaye, nje kidogo ya mji wa Tarime, Waziri Nyansaho alimwakilisha Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba. Pamoja na ujumbe wake, walichangia shilingi milioni 82.

Washiriki kutoka makanisa mbalimbali ya SDA ndani ya jimbo hilo pamoja na wadau wengine walifanikiwa kuchangia shilingi milioni 559, na kufikisha jumla ya makusanyo kuwa milioni 641.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Nyansaho alieleza kufurahishwa na mwitikio mkubwa wa waumini na wadau, akisema hali hiyo ni ishara kuwa ujenzi wa ofisi hiyo utakamilika kwa mafanikio.


“Inaonekana nimekuja na mibaraka, kwa jinsi matoleo ya leo yalivyokwenda, ujenzi wa jengo la ofisi ya SDA North Mara Field utakamilika na jengo litasimama,” alisema Waziri Nyansaho.



Katika hafla hiyo, Waziri Nyansaho aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo mfanyabiashara maarufu wa Kanda ya Ziwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Mkoa wa Mara, Christopher Mwita Gachuma, Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele.


Kwa upande wake, Askofu wa SDA Jimbo la North Mara Field, Dkt. Benjamin Ngalama Biha, alimshukuru Waziri Nyansaho na viongozi wengine kwa kushiriki na kuchangia katika harambee hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa katika hafla hiyo, ujenzi wa jengo la ofisi ya jimbo hilo utakuwa wa ghorofa mbili na unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka huu. Mradi huo unakadiriwa kugharimu jumla ya shilingi bilioni 3.5.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post