Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome, Manispaa ya Shinyanga,
Solomon Nalinga Najulwa maarufu Cheupe, ametoa wito kwa wakazi wa mtaa huo
kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa ulinzi na usalama ili kudumisha amani
iliyopo.
Akizungumza na Misalaba Media, Najulwa amewashukuru na
kuwapongeza wananchi wa mtaa huo kwa kuendelea kulinda amani na utulivu,
hususan katika kipindi cha Sikukuu ya Pasaka, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza
hali hiyo katika maisha ya kila siku.
Amesema kuwa ushirikiano wa wananchi katika masuala ya
ulinzi na usalama umekuwa chachu ya mafanikio ya mtaa huo, huku akiwahimiza
kuendelea kushirikiana na vyombo vya dola ili kuhakikisha mazingira yanaendelea
kuwa salama.
Aidha, Mwenyekiti huyo ametumia nafasi hiyo kuwataka
vijana wanaotafuta ajira katika makampuni mbalimbali, hasa ndani ya Mkoa wa
Shinyanga, kufika katika ofisi yake ili waweze kuandikiwa barua za utambulisho
zitakazowasaidia kupata ajira kwa urahisi na kuepuka changamoto zisizo za
lazima.
Sambamba na hilo, amewahimiza wakazi wa mtaa huo
kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo, huku akiwataka vijana
kujiepusha na makundi yasiyofaa yanayoweza kuharibu ndoto zao na mustakabali
wao.
Kwa upande wao, baadhi ya vijana wa mtaa huo akiwemo
Njile Kumalija na Emmanuel Mbeja, wameahidi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa
amani na kushiriki kikamilifu katika kudumisha usalama wa mtaa huo pamoja na
taifa kwa ujumla.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment