Katika kutekeleza Malengo ya Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ikiwamo lengo la Asilimia 80 ya Watanzania wanatumia Nishati Safi ya kupikia ifakapo 2034, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza kutekeleza mradi wa kusambaza majiko banifu zaidi ya 10, 300 kwa Wananchi mkoani Tabora
Akizungumza leo Aprili 11 wakati wa kutambulisha mtoa huduma, Kampuni ya Burn manufacturing Tanzania Ltd. aliyeshinda zabuni ya kusambaza majiko hayo kwa mkoa wa Tabora, Mhandisi Miradi kutoka REA, Ramadhan Mganga amesema Serikali kupitia REA imetoa kiasi cha shilingi 641,291,596 kwa ajili ya ruzuku ya majiko hayo kwa Mkoa huo.
“Dhamira ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuendelea kuboresha maisha ya wananchi pamoja na kulinda mazingira kwa kuhakikisha nishati safi za kupikia zinapatikana kwa bei nafuu zaidi na ndio maana akaridhia kutoa fedha kama ruzuku katika majiko haya.
Majiko haya kwa bei ya kawaida ni shilingi 62,000 mpaka shilingi 70,000 lakini serikali imeweka ruzuku ya asilimia 80, hivyo mwananchi atalipia kiasi cha shilingi 12,500 tu kuweza kupata jiko hili na kiasi kilichobaki serikali inalipia,” amesema Mhandisi Mganga.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, CPA. Amos Ackim amesema kuwa wamejipanga pamoja na watendaji katika Wilaya zote 6 za Mkoa huo zitakazonufaika na mradi huo kuhakikisha wananchi waliokusudiwa wanafikiwa na malengo ya mradi huo yanafikiwa.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Mhe. Mohamed Mtulyakwaku amewahamasisha wananchi kuendelea kuunga mkono kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kununua majiko banifu ambayo ni rafiki kwa mazingira na ni rafiki pia kwa afya ya anayetumia.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment