Msanii wa muziki wa Singeli Dogo Paten amefunguka kuwa bado ana nguvu kubwa ya kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki, akiahidi kuendelea kutoa ngoma kali zitakazowavutia mashabiki wake. Akizungumza na Misalaba Media, Dogo Paten amesema uwezo wake hauishii Singeli pekee bali anaweza pia kufanya Bongo Fleva, jambo linalompa nafasi ya kuonesha ubunifu mpana zaidi.
Aidha, amewataka mashabiki wake kujiandaa kupokea kazi nyingi mpya alizozielezea kuwa ni kali na zenye ubora. Msanii huyo pia amesisitiza kuwa anawapenda na kuwathamini mashabiki wake, akitoa shukrani maalum kwa wakazi wa Shinyanga kwa kumpokea vizuri kila anapofanya maonesho yake, akiahidi kuendelea kuwapa burudani ya kiwango cha juu.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment