" FUNGUNI SEKONDARI YATOA MOTISHA KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI

FUNGUNI SEKONDARI YATOA MOTISHA KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI


NA: MWANDISHI WETU, PANGANI Katika kuhakikisha ari ya wanafunzi kusoma inaongezeka na kuongeza ufaulu wa shule, uongozi wa Shule ya Sekondari Funguni ya wilayani Pangani mkoani Tanga, imetoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kawa kupata Daraja la Kwanza katika Mitihani ya Robo Muhula wa Kwanza kwa mwaka 2026Tukio la kukabidhi zawadi hizo, limefanyika Aprili 30, 2026, shuleni hapo ambapo wito umetolewa kwa wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu vizuri mitihani yao huku uongozi wa shule ukiahidi kuendelea kuwatambua wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani mbalimbali kwa kuwapa motisha.Katika tukio hilo, Makamu Mkuu wa Shule, Masoud Abdallah, amesema wanafunzi wanapaswa kusoma kwa bidii ili kuweza kufikia ndoto zao za kimaisha kwani elimu ndiyo nyenzo ya kufikia malengo yao."Leo tunatoa zawadi kwa wanafunzi waliopata Daraja la Kwanza (Division One) kuanzia Kidato cha Kwanza Hadi Cha Nne, hii iwe chachu kwa wengine kusoma kwa bidii, malengo ya shule yetu ni kuhakikisha wanafunzi wote wanafaulu  ili waweze kuendelea na masomo," amesema Masoud.Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo, Chiku Iddy amesema wanafunzi wanapaswa kuongeza kasi ya ujifunzaji kwani dunia ya leo inahitaji watu wenye maarifa na ujuzi.Katika hatua nyingine, Mwalimu wa Michezo wa shule hiyo, Isihaka Shekalaghe amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii na wajiepushe na mahusiano ya kimapenzi kwani yanachangia kushusha ufaulu wa masomo.Wanafunzi waliofanya vizuri walikabidhiwa zawadi mbalimbali zikiwemo madaftari makubwa magumu (counter books) pamoja na kalamu za wino huku wakiahidi kufanya vizuri zaidi katika mitihani ijayo ikiwemo mitihani ya ndani, ya pamoja na hata ya kitaifa.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post