Na Mapuli
Kitina Misalaba
Katibu wa
AIC Kambarage Choir, Japhet Alex Bulugu amewahimiza Wakristo kutumia vizuri
majukwaa ya kidijitali kwa kusubscribe, kulike, kucomment na kushare video
mbalimbali za injili ili kusaidia kueneza neno la Mungu kwa watu wengi zaidi.
Bulugu
ametoa elimu hiyo leo Aprili 19, 2026 wakati wa ibada iliyofanyika katika
Kanisa la AICT Kambarage lililopo mjini Shinyanga, ambapo ameeleza kuwa
teknolojia imekuwa nyenzo muhimu katika kufikisha ujumbe wa injili kwa haraka
na kwa watu wengi zaidi.
Amesema
vitendo hivyo vinavyoonekana vidogo vina mchango mkubwa katika kusaidia kazi ya
Mungu kukua, kwani vinasaidia kuongeza uonekano wa maudhui ya injili kwenye
mitandao ya kijamii na kuwafikia watu ambao huenda wasingeweza kufika kanisani.
Kanisa la AICT Kambarage limeendelea kutumia fursa ya teknolojia kuwafikia waumini wake na jamii kwa ujumla kupitia mitandao ya kijamii, hatua inayochangia kukuza huduma na kuimarisha imani kwa waumini.

Katibu wa
AIC Kambarage Choir, Japhet Alex Bulugu akizungumza kwenye ibada ya leo
Jumapili Aprili 19, 2026.

Katibu wa AIC Kambarage Choir, Japhet Alex Bulugu akizungumza kwenye ibada ya leo Jumapili Aprili 19, 2026.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
Post a Comment