Wakristo
mkoani wameaswa kuwa wavumilivu wanapokumbana na changamoto mbalimbali za
maisha na kuendelea kumtegemea Mungu kama nguzo pekee ya matumaini yao, badala
ya kukata tamaa au kukimbilia msaada usio na tija.
Wito huo
umetolewa na Mchungaji wa Kanisa la AICT Kambarage, Jonas Mwita, katika ibada
ya Jumapili iliyofanyika leo Aprili 19, 2026, ambapo amesisitiza kuwa kipindi
cha shida au changamoto ni sehemu ya maisha ya kila mwanadamu, hivyo kinahitaji
imani thabiti na subira.
Amesema
Wakristo wanapaswa kumlilia Mungu katika nyakati za shida badala ya kutegemea
sana wanadamu, akieleza kuwa wakati mwingine binadamu wanaweza kushindwa kutoa
msaada wa kweli, au hata kugeuza matatizo ya wenzao kuwa mjadala usio na
msaada.
Ameongeza
kuwa uvumilivu ni silaha muhimu katika kushinda changamoto, akimtaja Ayubu kama
mfano wa mtu aliyepitia mateso makubwa lakini hakukata tamaa wala kuacha
kumtumaini Mungu, hali iliyomfanya hatimaye kushinda majaribu aliyokumbana
nayo.
Aidha,
amewatahadharisha waumini kujiepusha na ushauri mbaya unaoweza kuwakatisha
tamaa au kuwapeleka mbali na imani yao, akisisitiza kuwa si kila ushauri
unaotolewa katika jamii unaleta manufaa.
Mbali na
hilo, ujumbe huo pia umegusa jamii kwa ujumla, ukihimiza watu wote kujenga moyo
wa kuvumiliana, kusaidiana na kutunza siri za wenzao wanapopitia nyakati ngumu,
badala ya kubeza au kuwakatisha tamaa.
Kanisa la AICT Kambarage limeendelea kuwa chanzo cha faraja na mwongozo wa kiroho kwa waumini na jamii, likitoa mafundisho yanayolenga kujenga moyo wa uvumilivu, upendo na mshikamano miongoni mwa watu.
Mchungaji wa
Kanisa la AICT Kambarage, Jonas Mwita, akihubiri katika ibada ya leo Jumapili Aprili
19, 2026.
Mchungaji wa
Kanisa la AICT Kambarage, Jonas Mwita, akihubiri katika ibada ya leo Jumapili Aprili
19, 2026.
Elikana Wallace, akiongoza ibada ya leo Jumapili Aprili 19, 2026.

Katibu wa kanisa la AICT Kambarage, Maligisa James Dotto akisoma matangazo ya kanisa kwenye ibada ya leo Jumapili Aprili 19, 2026.
Katibu wa kanisa la AICT Kambarage, Maligisa James Dotto akisoma matangazo ya kanisa kwenye ibada ya leo Jumapili Aprili 19, 2026.
Akina Mama kwaya wakiimba katika ibada ya leo (Aprili 19, 2026) Jumapili kwenye kanisa la AICT Kambarage.
Akina Mama kwaya wakiimba katika ibada ya leo (Aprili 19, 2026) Jumapili kwenye kanisa la AICT Kambarage.
AIC Kambarage Choir wakiimba leo Aprili 19, 2026 kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa la AICT Kambarage

Katibu wa
AIC Kambarage Choir, Japhet Alex Bulugu akizungumza kwenye ibada ya leo
Jumapili Aprili 19, 2026.

Post a Comment