" MALORI YANAYOKWEPA USHURU YADAIWA KUHARIBU BARABARA MWIKA KUSINI

MALORI YANAYOKWEPA USHURU YADAIWA KUHARIBU BARABARA MWIKA KUSINI

Na Mwandishi WetuMoshiBarabara zenye urefu wa kilomita 64 zilizojengwa kwa nguvu za wananchi na wadau, wa maendeleo katika kijiji cha Kiruweni kata ya Mwika Kusini wilaya ya Moshi zipo hatarini kuharibika baada ya malori yenye vifaa vya ujenzi kuzitumia kama njia ya ukwepaji ushuru.Baadhi ya malori ambayo hubeba vifaa hivyo kama mchanga,mawe,kokoto, na matofali kutoka wilaya ya Rombo eneo la Holili huzitumia kama njia ya ukwepaji wa ushuru wa halmashauri na pia kukwepa kupitia katika mizani.Mwenyekiti wa kitongoji cha Kiruweni kati Jackson Machang'u amesema kuwa ipo haja ya mamlaka husika kuangalia upya jambo hilo kwani linasababisha hasara mara mbili ikiwemo kuharibu barabara lakini pia kuikosesha halmashauri mapato.Amesema kuchelewa kudhibiti malori hayo kunaenda kuleta athari kubwa zaidi ikiwemo kuharibu barabara hizo zilizojengwa kwa nguvu za wananchi kwani hubeba mzigo mkubwa tofauti na viwango vilivyowekwa kisheria."Ipo haja ya mamlaka zinazohusika sasa kuona hili tatizo kwa sababunkwa siku sio chini ya malori 60 hadi 70 yanapita hivyo inaweza kuona ni nanma gani tatizo lilivyo kubwa katika eneo letu hili'amesemaJohn Tarimo diwani wa kata ya Mwika Kusini amesema kuwa tayari ameshapata malalamiko hayo na kuwa tayari ameshayafikisha kwa mamlaka husika ili kuweza kuchukuliwa kwa hatua kabla athari hazijawa kubwa zaidi ya hivi sasa.Amesema ukweli ni kuwa barabara hizo zinapoharibika tatizo litabaki palepale kama ilivyo kuwa mwanzoni na kuwa kama sehemu ya kijiji hawezi kukubali kuona jitihada za wanançhi hao zinakwamisha kwa maslahi ya watu wachache'Ikumbukwe tulitumia muda na fedha nyingi katika mradi huu wa barabara sasa maslahi ya wachache yasituharibie na kuturudisha kule tulipotoka mwanzoni'amesemaMwisho

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post