" MCHUNGAJI JONAS MWITA AWAHIMIZA WAKRISTO KUWA MABALOZI WA AMANI

MCHUNGAJI JONAS MWITA AWAHIMIZA WAKRISTO KUWA MABALOZI WA AMANI



 Mchungaji wa Kanisa la AICT Kambarage, Jonas Mwita, amewahimiza Wakristo kuwa mfano bora katika jamii kwa kusimamia na kulinda amani katika maeneo yao.

Mchungaji Mwita amesema kuwa kila Mkristo ana wajibu wa kuhakikisha anachangia kudumisha utulivu na mshikamano, akibainisha kuwa amani ni msingi muhimu wa maendeleo ya jamii.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Wakristo kuchagua marafiki na watu wanaowazunguka, ili kuepuka ushawishi wa ushauri mbaya unaoweza kuwapeleka katika matendo yanayohatarisha amani na mustakabali wao.

Aidha, amewahimiza waumini kuendelea kushikamana, kuheshimiana na kuzingatia maadili mema katika maisha yao ya kila siku, akieleza kuwa jamii yenye hofu ya Mungu huwa na msingi imara wa amani na upendo.

Mchungaji Mwita ametoa rai kwa Wakristo na jamii kwa ujumla kuendelea kuwa walinzi wa amani kwa vitendo, ili kuhakikisha utulivu unaendelea kudumu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post