
Na Paul KayandaKahamaAprili 19, 2026Zaidi ya wachimbaji wadogo 6,000 wa dhahabu katika mgodi wa Nyamishiga, uliopo Kata ya Lunguya wilayani Kahama, wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kwa kuwapatia leseni za uchimbaji wazawa, hatua iliyowaondolea hofu ya kufukuzwa na kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa uhakika.Wakizungumza juzi, wachimbaji hao walisema awali walikuwa wakifanya kazi katika mazingira ya wasiwasi kutokana na kukosa uhalali. Hata hivyo, baada ya kurasimishwa na kupatiwa leseni, sasa wanafanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za sekta ya madini pamoja na kulipa mapato ya Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali.Meneja wa mgodi wa Nyamishiga, Hosea Mbusule, alisema mgodi huo una zaidi ya wachimbaji wadogo 6,000 walioajiriwa na kujiajiri. Alieleza kuwa wanaishukuru Serikali chini ya Rais Samia pamoja na Wizara ya Madini inayoongozwa na Waziri Anthony Mavunde kwa kuweka mazingira rafiki ya kazi, akibainisha kuwa kabla ya kupatiwa leseni walikuwa na hofu ya kuwekeza.Aliongeza kuwa baada ya kupatiwa leseni, si wachimbaji pekee wanaonufaika bali pia jamii inayozunguka mgodi huo, ikiwemo wakulima na watoa huduma mbalimbali, ambao sasa wanashuhudia ongezeko la shughuli za kiuchumi.Kwa upande wake, mmoja wa wachimbaji hao, Merania Nyanda, alisema hatua hiyo imewaongezea ari ya kuwekeza zaidi katika shughuli za uchimbaji. Aliwataka wanawake kujitokeza kushiriki kikamilifu katika sekta hiyo, akisisitiza kuwa uchimbaji si kazi ya wanaume pekee kwani wanawake pia wana uwezo wa kufanya vizuri.Naye Mwenyekiti Mkuu wa Chama cha Wakaguzi wa Usalama Migodini (CHAUMITA), Shija Mussa, alisema mgodi huo una takribani miezi sita tangu kugunduliwa kwa dhahabu. Alibainisha kuwa wakaguzi wamejipanga kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa kuzingatia usalama pamoja na kufuata sheria na miongozo ya Tume ya Madini.Mussa aliipongeza Wizara ya Madini chini ya Waziri Mavunde kwa kuendelea kuwawezesha wachimbaji na wawekezaji wazawa kwa kuwapatia leseni, jambo linalowawezesha kunufaika na rasilimali za taifa kwa njia halali na endelevu.Aidha, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyamishiga, Lugwisha Lulenganija, alisema kurasimishwa kwa wachimbaji kumeleta mabadiliko chanya katika kijiji hicho, ikiwemo kuongezeka kwa mapato ya wananchi na kuboreshwa kwa hali ya maisha. Aliahidi kuendelea kushirikiana na mamlaka husika ili kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa amani na utulivu.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment