" MKAKATI WA KUZIBA UFA WA KITAIFA: KWANINI TUME INAENDELEA KUONGEA NA WANANCHI?

MKAKATI WA KUZIBA UFA WA KITAIFA: KWANINI TUME INAENDELEA KUONGEA NA WANANCHI?


Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman amesema tume hiyo kazi yake ilikuwa kubaini hoja kutokana na ushahidi uliowasilishwa.

Jaji Chande, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, Jumanne Aprili 28, 2026 alipozungumza na wahariri na waandishi wa habari.

"Tume kazi yake ya msingi ilikuwa ni kubaini hoja na kubaini hoja ni fact finding kutokana na ushahidi uliowasilishwa mbele ya tume. Kujibu zile hadidu za rejea tulizopewa," amesema.

Tume imeweka wazi kuwa yenyewe si kama mahakama inayofunga jalada baada ya hukumu, bali ni chombo cha kurekebisha jamii ambacho kina wajibu wa kuelimisha umma kuhusu vihatarishi vya amani kama ukosefu wa ajira kwa vijana na suala la utekaji. 

Kazi ya tume sasa ni kutoa tiba ya kisaikolojia na kisheria kwa taifa kwa kuonesha mapungufu ya kijamii yaliyotumiwa na watu wenye nia ovu kuwasajili vijana katika vurugu. 

Hii ni hatua ya makusudi ya kuhakikisha kuwa "ufa" uliopo unazibwa ili kuzuia hatari ya kujenga upya machafuko, jambo ambalo haliwezi kueleweka na watu wanaofurahia kuona nchi ikiingia katika taharuki kupitia habari za uongo na ukosoaji usio na tija.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post