Kishindo cha ripoti hii kimejikita katika ukweli mchungu kuwa vurugu za mwaka 2025 hazikuwa za bahati mbaya bali ni mpango mkakati uliokusudiwa uliokuwa na mbinu zaidi ya 16 za utekelezaji.
Aidha Mjumbe wa tume ambaye ni IGP mstaafu Said Mwema aliwataka Watanzania kutokuwa na shaka na ripoti ya tume kwa sababu wananchizaidi ya 63,000. waliokutana nao kwa njia mbalimbali .
Alisema hayo wakati tume ilipokutana na wahariri na waandishi wa Habari kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Aprili 28..
“Kuna watu wa bodaboba, mama lishe na vikundi mbalimbali walikiri mbele ya tume kushiriki kwa namna moja au nyingine na wengine walikiri kupewa fedha kwa ahadi ya kazi maalum,” aliongeza.
Alieleza kuwa matukio na picha mbalimbali pamoja na ushahidi mwingine ulionesha kuwa vurugu hizo zilipangwa mbinu zaidi ya 16 ili jambo hili liweze kufanikiwa.
Kupitia ushahidi wa moja kwa moja kutoka kwa zaidi ya watu 62,700, wakiwemo makundi ya bodaboda na mama lishe waliokiri kupewa fedha kwa ajili ya kufanya uhalifu, tume imeziba nafasi ya uzushi unaovumishwa na watu maarufu mitandaoni.
Huku kejeli zikitawala kwenye "picha mjongeo" ambazo nyingi zimebainika kuwa ni za matukio ya nje ya nchi, Tume ya Jaji Chande imetumia wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi kubaini ukweli dhidi ya propaganda.
Ni hatari kwa taifa pale wananchi wanapoamini kila kinachopita kwenye simu zao bila kuchuja, na hapa ndipo tume imejipambanua kwa kuonesha kuwa ushahidi wa viapo na nyaraka unashinda kelele za mitandao ambazo hazina msingi wa kijamii wala kisheria.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment