" UHURU WA TUME NI ZAIDI YA JESHI LA POLISI: JIBU KWA WANAOHOJI UTENDAJI KAZI WA JAJI CHANDE

UHURU WA TUME NI ZAIDI YA JESHI LA POLISI: JIBU KWA WANAOHOJI UTENDAJI KAZI WA JAJI CHANDE

Dhana potofu inayojengwa na wadhihaki mtandaoni kuwa tume ilitegemea taarifa za Jeshi la Polisi pekee imesambaratishwa na ukweli wa kitakwimu uliowekwa wazi na Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kuchunguza Vurugu za wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025  Jaji Mohamed Chande Othman. 

Katika hali inayoonesha weledi wa hali ya juu, tume ilikusanya viapo 953 kutoka kwa raia wa kawaida dhidi ya viapo 26 tu kutoka kwa askari polisi, ikiwa ni uthibitisho tosha wa namna ilivyotoa nafasi pana kwa waathirika na wananchi kuliko vyombo vya dola. 

Hatua ya tume kutembelea mikoa 11 na kufanya mahojiano ya ana kwa ana na maelfu ya watu ni kielelezo kuwa ripoti hii ni sauti ya umma na si sauti ya serikali kama inavyodaiwa na wasioitakia mema nchi. 

Hayo yalielezwa na wajumbe mbalimbali wa tume hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake  Jaji Mohamed Chande Othman. ilipokutana na wahariri na waandishi wa Habari kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Aprili 28.

Hivyo, wale wanaojaribu kupunguza thamani ya kazi hii wanashauriwa kurejea kwenye takwimu hizi ili waone namna tume ilivyochimbua mizizi ya matatizo badala ya kuangalia mambo kwa juu juu kama wafanyavyo wachambuzi wa vijiwe vya kidijitali.

Naye Mjumbe wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu 2025, Jaji Mkuu Mstaafu Profesa Ibrahim Juma amesisitiza kuwa maoni ya kupinga ripoti yanapaswa kujikita katika mbinu za uchambuzi (methodolojia) na vyanzo halisi, kama ilivyofanywa na tume, badala ya hoja zisizo na msingi wa kitaalamu.

Ameeleza kuwa Tume ilifanya kazi kwa kufuata taratibu za kitaaluma na ushahidi wa kina, hivyo ukosoaji unapaswa kuzingatia viwango hivyo ili kuwa na tija.

Aidha, amebainisha kuwa tume ni huru kwa mujibu wa kiapo na utekelezaji wa hadidu za rejea, jambo linalotofautisha matokeo yake na maoni ya kawaida ya wananchi wengine.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post