Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde.Paul Kayanda, KahamaMWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Busulwangili, Kata ya Bulyanhulu katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Maxmiliani Buchanagandi, amewataka wananchi kuacha kuhamasisha vurugu na kujichukulia sheria mkononi wakati Mwekezaji Wa mgodi WA Isunda analengo la kuleta maendeleo kwenye Kijiji chao, akisisitiza kuwa vitendo hivyo vinachochea uvunjifu wa amani katika jamii.Buchanagandi alitoa wito huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia mgogoro unaoendelea kati ya mmiliki wa leseni ya Mgodi wa Isunda na baadhi ya wananchi wenye mashamba katika eneo hilo.Alisema serikali ya kijiji inamtambua kisheria mwekezaji huyo mwenye leseni ya uchimbaji, na kuwataka wananchi kufuata taratibu halali za kudai haki zao badala ya kuchochea migogoro inayoweza kuhatarisha usalama wa watu na mali zao.“Ni muhimu kwa wananchi na wenye mashamba kuzingatia sheria na taratibu zilizopo. Serikali ipo tayari kusimamia haki, lakini si kwa njia ya vurugu,” alisema Buchanagandi.Aidha, aliwataka wahusika wa mgogoro huo kukaa mezani kwa mazungumzo ya amani chini ya usimamizi wa serikali ya kijiji ili kupata suluhisho la kudumu.Kwa upande wao, baadhi ya wenye mashamba wameeleza kuridhishwa na mchakato wa fidia. Mmoja wao, aliyejitambulisha kwa jina la Mathias Katemi, alisema walikubaliana na mmiliki wa leseni baada ya kuelezwa kuhusu mpango wa kubadilisha uchimbaji kutoka mdogo kwenda wa kisasa, na tayari amelipwa fidia.Naye Masumbuko Misalaba alisema walishirikishwa kikamilifu na serikali ya kijiji pamoja na mwekezaji, na kukubaliana kupisha eneo hilo baada ya kulipwa fidia stahiki.Hata hivyo, mmiliki mwingine wa shamba linalodaiwa kuwa na Madini ya dhahabu Joseph Kalemela, ambaye anamiliki hekari 47.2 za ardhi, ameendelea kupinga uwekezaji huo akisema kuwa licha ya kufanyiwa tathmini ya mali zake na kupewa kiasi cha shilingi milioni 200 kama fidia, amekataa kupokea fedha hizo.Akizungumza kwa niaba ya wenye leseni ya uchimbaji Madini PLM 0253, Meneja wa Mgodi wa Isunda, Gehonde Mataso, alisema wamezingatia taratibu zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wananchi na kulipa fidia kwa waliokubaliana.Mataso alisema changamoto iliyopo ni kwa baadhi ya wananchi wachache, akiwemo Kalemela na wenzake wawili, ambao wameendelea kupinga mradi huo na kudaiwa kuhamasisha vurugu zinazoathiri amani na maendeleo ya eneo hilo.Alisema kuwa kampuni ya Sunda bado inaendelea kulipa fidia Kwa wamiliki wa shamba na hivi karibuni zoezi hilo linakwenda kukamilika licha ya Mzee Kalemela kuendelea kusimamia msimamo Wa kukataa kulipwa fidia ya shilingi milioni 200 Ili apishe Kama wenzake ambao hawajaleta usumbufu. Hata hivyo katikà kikao chake na wadau wa sekta ya Madini kilichoketi April 14,2026 Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameagiza kusimamishwa kwa shughuli za uchimbaji wa Madini katika kijiji cha Busulwangili, wilayani Kahama, kufuatia mgogoro kati ya Kikundi cha Isunda, wamiliki wa mashamba na maduara. Hatua hiyo inalenga kutoa nafasi ya uchunguzi wa kina juu ya uhalali wa umiliki na uwekezaji.Amesema shughuli zote zitasimama hadi mchakato wa ubia na makubaliano kati ya pande husika utakapokamilika na kuthibitishwa rasmi. Serikali inalenga kuhakikisha haki inatendeka kwa kila upande bila upendeleo.Waziri Mavunde pia ametoa muda wa siku 3 kwa wadau husika kuwasilisha nyaraka muhimu zitakazosaidia kutatua mgogoro huo kwa njia ya kisheria na yenye uwazi.Aidha, amesisitiza kuwa sheria ya madini inapaswa kufuatwa kikamilifu, hususan kuhusu haki ya kwanza kwa wamiliki wa maduara kabla ya kuingiza wawekezaji wengine.Kwa upande mwingine, amewataka wadau wote wa sekta ya madini kuacha migogoro isiyo ya lazima na badala yake kushirikiana kwa kuzingatia sheria, uwazi na uwajibikaji ili kuimarisha sekta hiyo.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment