Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga,
Bwana John Siagi, amewakumbusha viongozi wa Seneti Mkoa wa Shinyanga kuendelea
kuwa mabalozi wazuri wa kusimamia amani na utulivu katika maeneo yao.
Siagi ametoa wito huo wakati wa kikao cha pamoja,
ambapo ameeleza kwa ufupi historia ya Tanzania tangu ilipopata uhuru na namna
ilivyoendelea kuwa nchi ya amani, akibainisha kuwa hali hiyo imejengwa na
viongozi mbalimbali wakiwemo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Amesema kuwa amani iliyopo nchini ni tunu muhimu
inayopaswa kulindwa na kila Mtanzania, huku akisisitiza kuwa viongozi wa
serikali wameendelea kuisimamia kwa ufanisi na kuhakikisha inaendelea kudumu.
Aidha, amesema Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga
itaendelea kushirikiana na viongozi mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao,
ikiwa ni pamoja na kuendeleza amani kwa mujibu wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Seneti Mkoa wa
Shinyanga, Bwana Jackson Aloyce Mwizarubi, amesema yeye pamoja na viongozi
wengine wa Seneti wataendelea kusimamia sheria na taratibu za nchi ili
kuhakikisha amani inalindwa wakati wote.
Ameongeza kuwa endapo kutajitokeza viashiria vyovyote
vya uvunjifu wa amani, watatoa taarifa kwa mamlaka husika ili hatua za kisheria
ziweze kuchukuliwa mapema.
Mwizarubi pia amebainisha kuwa kuanzia Aprili 17,
2026, viongozi wa Seneti Mkoa wa Shinyanga wameanza ziara ya kutembelea vyuo
mbalimbali mkoani humo, kwa lengo la kuwasaidia vijana kutambua fursa zilizopo,
kusikiliza changamoto zao na kuimarisha uongozi katika ngazi za matawi.
Kwa pamoja, viongozi hao wamehimiza vijana na wananchi kwa ujumla kuendelea kulinda amani, kuheshimu sheria na kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kudumisha ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment